SWALI:
Assalam Alaykum warahmatul - llahi wabarakat.
Naomba kujua tofauti ya hadithi hizi mbili. Amesema mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam: Mwenye kusoma aya mbili za mwisho wa suratul-baqarah Mara mbli baaye ya swala ya Isha (basi) Zinamtosheleza. kwa ibada ya usiku mzima. Vipi kumtosheleza huko. Na hadithi myingine inasema pia amesema? Mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam anayesoma aya mbili za mwisho wa suratul-baqarah usiku zinamtosheleza. Ipi ni sahihi
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Qiyaamah.
Hadiyth ya kwanza uliyotaja kuwa ni kusoma Aayah mbili baada ya Swalah ya 'Ishaa hatukuipata katika Hadiyth zinazojulikana kuwa ni Sahiyh. Ama Hadiyth Sahiyh kwa maudhui hii ambayo imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim ni ile iliyosimuliwa na Ibnu Mas'uud Al badry [Radhia Allahu 'anhu]
من قرأ بالآيتين من آخر سورة البقرة في ليلة كفتاه
"Mwenye kusoma aya mbili za mwisho za suratu-Baqarah usiku zinamtosheleza".
Hadiyth hii ina maana kwamba inamtosheleza na shari za kila aina kama kukumbwa na majini, au shari ya aina yoyote nyingine na hubakia katika kinga usiku huo mzima hadi asubuhi.
Vile vile kusoma Aayatul-Kursiy pia ni kinga ya Muislamu pamoja na du'aa nyingine za kusoma kabla ya kulala ambazo ziko katika kitabu cha Hiswnul-Muslim kinachopatikana humu ndani ya Alhidaaya katika viungo vifuatavyo:
Na Allaah Anajua zaidi