ELIMU YA DINI YA KIISLAMU



©IIMEC.09
                                                                             .                             
Bismillahir Rahmaanir Rahyim

INTER ISLAMIC MOCK EXAMINATIONS COMMITTEE
CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION

FORM IV MOCK EXAMINATION

015/1                 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU-1


Muda:   Saa 2 ½                            Jumatatu, 3 Agosti, 2009 mchana                                                  
MAAGIZO:
1.            Mtihani huu una sehemu A, B, C, D na E.
2.            Jibu maswali YOTE.
3.            Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.
4.            Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.
5.            Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kitabu chako cha kujibia.
6.            Fuata kwa makini maelekezo ya kila swali.


Mtihani huu una kurasa 6 zenye maandishi



SEHEMU A
SUNNAH NA HADITHI  (Alama 10)

1.       Katika swali (i) – (x) chagua jibu lililo sahihi zaidi na uandike herufi yake katika karatasi yako ya kujibia.

(i)            Maana ya Sunnah katika Istilahi ya Kiislamu ni:
A.            Hadithi za Mtume (s.a.w)
B.            Mafundisho ya Maswahaba
C.            Matendo ya Mitume wa Allah
D.            Matendo ya Mtume (s.a.w.) ambayo ni sehemu ya Utume wake

(ii)           Ni muhimu kufuata Sunnah ya Mtume (s.a.w.) kwa sababu:
A.            Huwezi kuelewa Qur’an bila kufuata Sunnah
B.            Kilichoanza wakati wa Mtume ni Sunnah kisha Qur’an
C.            Sunnah inaelezea hadithi za Mtume
D.            Huwezi kumtii Mtume bila kumtii Allah

(iii)          Ni wakati upi katika historia ya uandishi wa hadithi ambapo uandishi wa hadithi ulistadi kuliko zote?
A.            Wakati wa Mtume
B.            Wakati wa Maswahaba
C.            Wakati wa Tabiina
D.            Wakati wa Tabii Tabiin

(iv)          Ni kigezo kipi kati ya hivi vifuatavyo hutumika kuitambua hadithi sahihi au dhaifu?
A.            Hadithi kutopingana na kauli ya Tabii Tabiin
B.            Hadithi kutopingana na Qur’an
C.            Ukamilifu wa matin na Isnad
D.            Ukamilifu wa Isnad

(v)           Kufuata madhehebu, rai au maoni kibubusa bila ya kutumia akili hujulikana kama
A.            Taqtiid
B.            Makahd
C.            Tajwiid
D.            Wahhid

(vi)          Hadithi zinazoanza kusimuliwa na Mtume (s.a.w.) yakiwa yakiwa ni maneno ya Allah (s.w.) lakini si Qur’an hujulikana kama:
A.            Hadithi Nabawiyyi
B.            Hadithi Qudusiyyi
C.            Hadithi Ahad
D.            Hadithi Matawatir

(vii)         Kitabu kipi katika hivi vifuatavyo kinachukua daraja ya kwanza ya usahihi kuliko vingine?
A.            Jamiu At Tirmidh
B.            Sahihi Al- Bukhar
C.            Sahihi Al-Muslim
D.            Sanad ya Ibn-Majah

(viii)        Kazi kubwa ya kwanza ya uandishi wa hadithi iliyoonekana katika kipindi cha maswahaba ilikuwa Al-qatadaya ya:
A.            Malik bin Anas
B.            Imam Bukhari
C.            Hazrat Ali
D.            Abu Huraira




(ix)          Msururu wa wapokezi tokea aliyemuona au kumsikia Mtume (s.a.w.) hadi kufikia aliyepokea na kuandika hadithi hujulikana kama:
A.            Rawi
B.            Matin
C.            Isnad
D.            Jamiu

(x)           Kipi kati ya vipengele vifuatavyo ni kipengele cha mambo yenye kuangamiza?
A.            Kukimbia siku ya vita vya jihadi
B.            Kutofuata sunnah za Mtume (s.a.w.)
C.            Kutomtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi

D.            Kutoamrisha mema

SEHEMU B:     QUR’AN (Alama 15)
2.         Chagua kutoka orodha B kifungu cha maneno kinachowiana na kifungu cha maneno cha orodha A. Kifungu cha orodha B kinaweza kuwianishwa zaidi ya mara moja.

ORODHA A:
(i)            “Na haikuwa kwa mtu kwamba Allah (s.w.) anasema naye ila kwa ilham au nyuma ya pazia au hutuma mjumbe naye humfunulia kiasi anachotaka”. [42:51]

(ii)           ….ni mwezi wa Ramadhani ambao ndani yake imeshuka hii Qur’an iwe uongozi kwa watu na hoja zilizowazi au uongozi na upambanuzi……. [2:185]

(iii)          Kwa yakini Mwenyezi Mungu amemhakikishia Mtume wake ndoto yake ya haki. [48:27]

(iv)          Ujumbe wa kwanza wa Qur’an kushushwa kwa Mtume (s.a.w.).

(v)           Chanzo cha elimu zote ni Allah (s.w.).

(vi)          Kuomba kuongozwa katika njia iliyonyooka ni wajibu kwa kila Muislamu.

(vii)         Uthman bin Affan (r.a.) amesema, wakati wowote Mtume wa Allah alipoteremshiwa wahyi humuita mmoja wa watu waliochaguliwa kuandika. (Tirmidh).

(viii)        “Na Qur’an tumeigawanya sehemu mbalimbali uwasomee watu kwa kituo na tumeiteremsha kidogo kidogo. [17:106]

(ix)          Allah ndiye chimbuko la kila fani ya elimu.

(x)           Kipambanuzi cha haki na batili.

(xi)          Allah ndiye chimbuko la kila fani ya elimu.

(xii)         Mwanadamu anahitajika kujikinga kwa Mola wake tu kutokana na shari ya viumbe.

(xiii)        “Ewe Mtume mbona unaharamisha alichokihalalisha Mwenyezi Mungu? Unataka radhi za wake zako ……”. [66:1]

(xiv)        Amemfundisha mwanadamu mambo aliyokuwa hayajui.

(xv)         Nabii Ibrahim (a.s.) alioteshwa kumchinja mwanae.

ORODHA B:
A.            Njia ya mawasiliano na Mwenyezi Mungu
B.            Lengo la Qur’an
C.            Alaq (96:1-5)
D.            Kuhifadhiwa Qur’an
E.             Qur’an ni neno la Allah
F.             Surat Falaq na Nnas
G.            Surat-Fat-ha au Al-hamdu
SEHEMU C:  TAWHIID (Alama 15)

3.         Panga vipengele vya (a), (b) na (c) katika mtiririko wenye kuleta mantiki majibu yaandikwe katika kijitabu cha kujibia.

Kwa mfano
Uislamu umesimamishwa juu ya nguzo tano zifuatazo:
(i)            Kutoa zaka
(ii)           Kuhiji Makka
(iii)          Kufunga Ramadhani
(iv)          Kutoa shahada mbili
(v)           Kusimamisha swala

Jibu ni (iv), (v), (iii), (i)

(a)           Wafuatao ni Mitume wa Allah:
(i)            Muhammad (s.a.w)
(ii)           Issa (a.s)
(iii)          Daud (a.s.)
(iv)          Daud (a.s.)
(v)           Suleyman (a.s.)

(b)           Sura ifuatayo inathibitisha umoja na upweke wa Mwenyezi Mungu:
(i)            Sema: Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja
(ii)           Wala hana anayefanana naye hata mmoja
(iii)          Ndiye anayestahili kukusudiwa
(iv)          Hakuzaa
(v)           Wala hakuzaliwa

(c)           Kisa kifuatacho kinathibitisha kuwa ufufuo ni jambo jepesi kwa Allah:
(i)            Kisha akamfufua akamuuliza ‘umekaa muda gani? Akasema nimekaa muda wa siku moja au sehemu ya siku (Mwenyezi Mungu) akasema: “Bali umekaa miaka mia, nawe tazama chakula chako na vinywaji vyako, havikuharibika.
(ii)           Basi alipopambanuliwa alinena “Najua kwamba Mwenyezi Mungu ni mwenye uweza juu ya kila kitu.
(iii)          Au kama yule aliyepita karibu na mji uliokuwa umekufa akasema “Mwenyezi Mungu anauhuisha vipi (mji) huu (na watu wake) baada ya kufa kwake.
(iv)          Na mtazame punda wako (amekuwa mifupa mitupu iliyo sagika). Na ili tukufanye uwe hoja kwa watu (ndio tumekufufua hivi). Na itazame mifupa (ya punda wako) jinsi tutakavyoinyanyua, kisha tukaivika nyama.
(v)           Basi Mwenyezi Mungu alimfisha kwa miaka mia.

SEHEMU D: FIQH (Alama 30)

4.         Jibu kwa ufupi kujaza nafasi zilizo wazi katika maswali la (i) – (xv). Andika neno au maneno yaliyokosekana tu katika karatasi yako ya kujibia.

(i)            Mwanadamu amekusudiwa kuwa ___________ wa __________ hapa ardhini.

(ii)           Ndio kiingilio cha Uislamu, tafsiri yake ni ______________________________________.

(iii)          Dharura za kisheria za kumfanya mtu kutokuswali ni _______________ na _______________.

(iv)          Ili pahali palipoingia najisi hafifu patatwaharike ni kwa ___________________ maji yaenee na kutiririka wakati kuondoa najisi ya kati na kati ni lazima kusafisha hadi _______iondoke.

(v)           Moja ya sharti za utoaji zakat ni __________________ kwa masimbulizi na miongoni mwa wanaostahiki kupewa zaka ni ___________________________________________.

(vi)          Kwa mujibu wa hadithi za Mtume (s.a.w.) miongoni mwa mambo yanayoharibu swaumu (funga) ni ________________________________________________________________________.

(vii)         Kutupa mawe kwenye Jamaratul Aqaba siku ya mwezi 10 Zulhija kunafutufnza ___________ na kusimama Arafa mwezi 9 Dhulhija kunatukumbusha __________________________________.

(viii)        Chemchem ya sheria ya Kiislamu ni _________________ na ___________________.

(ix)          Tofauti na mfumo wa Kidemokrasia, katika mfumo wa kisiasa wa Kiislamu ufalme wote ni wa _____________________ na hakuna __________________ aliyeko juu ya sheria.

(x)           Biashara inaweza kuwa ya haramu kwa kutofuata misingi aliyoiweka _________________ au biashara yenyewe ___________________ moja kwa moja.

(xi)          Moja ya kikwazo cha muoaji ni kuwa asiye na wake zaidi ya __________________ na wakati huo kwa muolewaji asiwe katika _____________ ya mume mwingine.

(xii)         Talaka ya “Zihar” kafara yake ni ____________ au _________________________________.

(xiii)        Sharti mojawapo la urithi ni kuwa na uhusiano wa ______________ au kwa ______________.

(xiv)        Moja ya makusudio ya ndoa katika Uislamu ni kuepusha jamii na _____________ katika familia __________________________________.

(xv)         Faida za swala ya jamaa ni kujenga ________________________ miongoni mwa Waislamu na kujifunza kanuni za ___________________________ wa Kiislamu.

SEHEMU E : TAREKH (Alama 30)

5.         Chagua neno au maneno (1-30) ili kukamilisha kauli (i-x) kwa usahihi.

Maneno/vifungu vya maneno
1.             Aqaba
2.             Hunain
3.             Maslahi binafsi
4.             Muta
5.             Kujielimisha
6.             Allah
7.             Qur’an
8.             Udhaifu wa imani
9.             Yathribu
10.          Khaibar
11.          Kuandika katiba
12.          Maquraish
13.          Vita vya Uhud
14.          Subra
15.          Dini
16.          Kuunganisha Ansari na Muhajirin
17.          Warumi
18.          Magumu
19.          Badri
20.          Uoni wa mbali
21.          Umma
22.          Ushirikina
23.          Huruma yake
24.          Maqamu Ibrahim
25.          Mwanadamu
26.          Manata
27.          Jina la Al-amin
28.          Upinzani
29.          Ibada
30.          Imani

MASWALI:

(i)            Kwa mujibu wa mafundisho ya Qur’an kila __________________ alipelekwa Mtume kwa lengo la kumuongoza _____________________________ katika njia iliyonyooka.

(ii)           Historia ya Makka ilipo Kaaba inadhihirishwa na ___________________________ na mahali Allah ameamrisha iwe sehemu ya _________________________________.

(iii)          Waarabu wa Makka wakati Qur’an inashushwa walibobea katika ____________________ na moja ya miungu yao ilikuwa _________________________________.

(iv)          _________________ na _________________ ni ushahidi tosha kuwa Muhammad (s.a.w.) tangu utotoni mwake alikuwa na tabia njema kabisa.

(v)           Baada ya wahyi wa kwanza na kuamrishwa ujumbe kwa watu wote Mtume Muhammad (s.a.w.) alikabiliana na _____________________ lakini aliendelea kufundisha __________________ sahihi ya kumuamini Allah.

(vi)          Tukio la Waislamu kutengwa katika bonde kwa miaka mitatu na kuuliwa baadhi ya maswahaba ni funzo kwetu kuwa katika kupigania _________ya Allah tuwe tayari kukabiliana na _____ yoyote.

(vii)         Mara tu Mtume (s.a.w.) alipofika Madina alifanya yafuatayo, kujenga Msikiti ___________ na ___________________.

(viii)        Maadui wa Dola ya Kiislamu Madina walikuwa _______________ Wayahudi, ________________ na Wanafiq.

(ix)          ____________________ ilikuwa Maquraishi wanalipiza kisasi baada ya kushindwa vibaya katika vita vya __________________.

(x)           ________________ na ___________ ni baadhi ya mazingitio kutokana na mkataba wa Hudaibiya

(xi)          Vita vya ____________ na vile vya _______________ ilikuwa ni ishara ya kukua na kuimarika kwa nguvu za kijeshi la dola ya Kiislamu.

(xii)         _______________ na ______________ vilichochea uasi dhidi ya dola ya Kiislamu wakati wa Ukhalifa wa Abubakar (r.a.).

(xiii)        Funzo kubwa kutokana na vita vya ______________ ni kuwa wingi si hoja na tunatakiwa tumtegemee ________________________ kila wakati.

(xiv)        Mikataba ya _____________________ kati ya Waislamu kuhamia Madina ____________ ndio ilipowafanya Waislamu kuhamia Madina.

(xv)         Ili kukabiliana na vikwazo dhidi ya Uislamu na Waislamu hawanabudi _________________ na kufuata _____________________ kwa mwongozo wa maisha.


WABILLAH TAWFIIQ