BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIIM
“SOMA KWA JINA LA ALLAH (S.W) UFAULU DUNIANI NA AKHERA”
NUKUU ZA SOMO
ELIMU YA DINI YA KIISLAMU
KIDATO CHA NNE
MADA ZA KIDATO CHA NNE
1.NGUZO ZA IMANI.
- Kuamini Mitume wa Mwenyezi Mungu.
- Kuamini siku ya mwisho.
- Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu.
2.MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA DINI.
- Makundi makuu ya Dini yaliyotajwa katika Qur’an.
3.CHIMBIKO LA FIQH
- Mgawanyiko wa madhehebu
4.FAMILIA YA KIISLAMU
- Ndoa katika Uislamu.
- Majukumu katika familia.
- Kudhibiti uzazi katika Uislamu.
- Talaka na Eda.
- Mirathi katika Uislamu.
- Hadhi na Haki za mwanamke katika Uislamu.
5.MFUMO WA JAMII YA KIISLAMU.
- Misingi na Maadili katika Uislamu.
- Sheria katika Uislamu.
- Uchumi katika Uislamu.
- Siasa na uendeshaji wa Dola.
6.QUR’AN
- Ithibati ya Qur’an
- Sura zilizoteuliwa (Tyn, Nashrah, Dhuha, A’alaa).
7.SUNNAH NA HADITH
- Hadith zilizoteuliwa.
8.HISTORIA YA UISLAMU BAADA YA KUTAWAFU MTUME (S.A.W) HADI HIVI LEO.
- Ukuaji na Uendeshaji wa Dola ya Kiislamu wakati wa Makhalifa wane waongofu.
- Uanzishwaji wa makundi ya harakati ya kuhuisha Uislamu ulimwenguni.
- Kuingia kwa Uislamu Tanzania na Afrika Mashariki.
NGUZO ZA IMANI.
Kuamini Mitume wa Mwenyezi Mungu.
Ushahidi wa kuwepo Mitume (a.s)
1. Katika Historia ya mwanadamu kulitokea watu waliodai kuwa ni Mitume wa Allah (s.w) na walionesha dalili mbalimbali za kuthibitisha utume wao.Mfano;
- Watu wa ‘Ad: Mtume Hud (a.s).
- Watu wa Thamud: Mtume Salehe (a.s).
- Ummah wa mwisho: Mtume Muhammad (s.a.w).
2. Qur’an imebainisha wazi kuwa Allah (s.w) aliwatuma Mitume (a.s) ili wasimamishe uadilifu katika jamii.Qur’an (57:25).
3. Jamii ya mwanadamu inakiri kuwa Mitume walikuwepo na walifanya kazi waliyotumwa na Allah (s.w).
Umuhimu wa kuamini Mitume wa Allah (s.w)
1.Ni nguzo ya nne (4) ya Imani ya kiislamu.Rejea Qur’an (2:136) na (2:285).
2.Ni amri ya Allah (s.w) kuamini Mitume wake na kuwatii.Qur’an (7:158).
3.Mwenye kukanusha nguzo hii hatabakia kuwa muislamu wa kweli bali atakuwa kafiri.(4:150-151) na (24:47-50).
4.Allah (s.w) ameahidi malipo makubwa sana kwa wale watakao waamini Mitume wake na kuishi kwa mujibu wa mafundisho yao.Qur’an (4:152) na (24:51-52).
Sifa za Mitume wa Mwenyezi mungu (s.w)
1.Walikuwa na upeo mkubwa wa Elimu.
2.Walikuwa wacha-Mungu kuliko watu wote katika nyakati zao.
3.Walikuwa na tabia njema kuliko watu wengine.
4.Walikuwa na sifa zote za ubinaadamu kama vile kula na kunywa.
5.Hawakuathiriwa na mazingira ya jamii zao.
Lengo la kuletwa Mitume (a.s)
Lengo la kuletwa Mitume (a.s) ni kuutawalisha Uislamu katika jamii ili jamii iishi maisha ya furaha na amani ya kweli.(57:25).
Mtume (s.a.w) .(9:33), (61:9) na (48:28).
“Kwa hakika Tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na tukaviteremsha vitabu na uadilifu pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu…” (57:25).
Lengo la kuletwa Mtume (s.a.w):
“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uongofu na dini ya haki ili ipate kuzishinda dini zote ijapokuwa washirikina watachukia”.(61:9).
Ni sababu gani zilizopelekea kuletwa Mtume baada ya kuondoka mwingine?
Huu
- Iwapo mafundisho ya Mtume aliyetangulia yamepotoshwa.
- Iwapo mafundisho ya mtume aliyetangulia hayakukamilika kiasi cha kutosheleza mahitaji yote ya binadamu ya kibinafsi na ya kijamii kulingana na wakati uliopo.
- Iwapo mtume aliyetangulia alipelekwa kwa watu wa taifa Fulani tu,hivyo ikabidi apelekwe mtume mwingine kwa taifa lililozuka.
Kwanini hapana haja ya kuja mtume mwingine baada ya Muhammad(s.a.w)?
- Qur’an imehifadhiwa na uharibifu wa aina yoyote,tangu mtume mwenyewe akiwepo na baada yake.Qur’an(41:42).
- Mtume Muhammad(s.a.w) ameletwa kwa walimwengu wote.
- Allah(s.w) ameukamilisha ujumbe wake kwa binadamu wakati wa utume wa Muhammad(s.a.w).(5:3).
Kwanini ujumbe wa Uislamu umekamilika na haupitwi na wakati?
- Mafundisho ya Uislamu ni ya milele kwa sababu ni ufunuo utokao kwa Mwenyezi Mungu mjuzi wa yote ya kale,ya sasa na yajayo,tena mwenye uhai wa milele.
- Uislamu umeegemeza mafundisho yake juu ya umbile la binadamu.Watu wote wamejengwa kwa majengo yale yale yaliyowajenga watu wa kale kabisa na hivyo umbile lao kimsingi ni lile lile.
- Uislamu umeweka utaratibu madhubuti unaoweza kuoanisha maendeleo ya binadamu na misingi ya kitabu cha Allah(Qur’an) na sunnah ya Mtume wake Muhammad(s.a.w).
Ni ipi maana halisi ya kuamini Mitume wa Allah (s.w) katika maisha ya kila siku?
- Kuwatii kwa kufuata maamrisho yao na kuacha makatazo yao katika kukiendea kila kipengele cha maisha ya kibinafsi na kijamii.Qur’an(3:31-32) na (59:7).
- Kuwafanya Mitume kuwa viigizo vya maisha ya binafsi,familia na jamii.Qur’an(33:21).
- Kuwapenda Mitume kuliko nafsi zetu.Qur’an(9:24).
- Kuwa na yakini kuwa Mtume Muhammad(s.a.w) ndiye mtume wa mwisho.Qur’an(33:40).
- Kumswalia Mtume(s.a.w) mara kwa mara na kila anapotajwa.Qur’an(33:56).
- Kuwafanya Mitume kuwa mahakimu pale tunapohitilafiana juu ya jambo lolote.Qur’an(4:65).
Kuamini siku ya mwisho.
Mazingira ya siku ya mwisho
Siku ya mwisho ni maisha yajayo ya milele baada ya maisha ya hapa duniani.
Zifuatazo ni hatua za siku ya mwisho:
(i) Kutokwa na roho
(ii) Maisha ya kaburini
(iii) Kufufuliwa na kuhudhurishwa mbele ya Allah (s.w) kwa hisabu.
(iv) Maisha ya milele ya peponi kwa watu wema na maisha ya motoni kwa watu waovu.
Madai ya makafiri dhidi ya kuwepo siku ya malipo na udhaifu wa madai hayo.
(i) Hapana uwezekano wa kupatikana uhai baada ya mtu kuoza na mifupa yake kusagika sagika.Qur’an(79:10-12) na (56:47).
Udhaifu
- Aliye muumba mwanadamu kwa mara ya kwanza hashindwi kumrudisha katika umbile lake la awali.
- Kuumba kwa mara ya pili ni kwepesi sana kuliko kwa mara ya kwanza,hivyo ufufuo utakuwa jambo jepesi.
- Aliye umba kwa mara ya kwanza hajachoka kiasi cha kushindwa kuumba mara ya pili.(Qur’an 50:15).
(ii) Waliokufa hawajarudi wakatoa ushahidi.Qur’an(45:25).
Udhaifu
- Katika utaratibu wa Allah(s.w) ufufuo hautakuwa wa mtu mmoja mmoja bali utakuwa kwa wote.Qur’an(56:49-50).
(iii) Kufa si lolote bali ni mtindo tu wa maisha ya ulimwengu.
Udhaifu
- Allah(s.w) ndiye aliye anzisha viumbe na ndiye atakaye virudisha.(30:27) kwani mwanadamu ametokana na nini?-tone la manii.
- Mwanadamu amepatikana kwa utaratibu madhubuti hatua kwa hatua na kifo ni katika hatua ya kuelekea maisha baada ya kufa.
- Mwanadamu ameumbwa kwa mara ya kwanza pasi na matashi yake ndivyo kufufuliwa kutakavyotokea bila ya matashi yake vilevile.
(iv) Mwanadamu hana lengo la maisha isipokuwa kustarehe tu.
Udhaifu
- Akili haikubali kuwa mwanadamu mwenye vipawa vya akili,ufahamu na utambuzi wa hali ya juu kuliko viumbe vyote lengo lake la maisha liishie kwenye kula,kunywa na kuishi kama wanyama.(Qur’an 44:38).
- Akili inatulazimisha tuone kuwa mwanadamu ametunukiwa vipaji vyote alivyonavyo na neema zote zilizomzunguka kwa lengo maalumu.(Qur’an51:56).
- Hapanabudi kuwepo siku ya malipo ili Yule aliyemtunukia mwanadamu neema zote alizonazo amuulize jinsi alivyozitumia neema hizo.Qur’an(102:8).
Hoja za kuthibitisha kuwepo siku ya malipo
- Wale waliofanya wema hapa duniani bila ya kupata ujira unaostahiki walipwe fadhila ya wema wao.Qur’an(55:60).
- Wale waliodhulumu haki za watu hapa duniani warudishe haki kwa wenyewe mbele ya hakimu wa mahakimu.Qur’an(95:8).
- Wale wababe waliofanya uovu uliokithiri hapa duniani bila ya kupata adhabu inayostahiki,wahukumiwe na kupewa adhabu inayolingana na makosa yao mbele ya Mfalme wa wafalme.Qur’an(1:4).
- Watu waulizwe vipi walitumia neema na vipaji mbalimbali walivyotunukiwa na muumba wao katika kuliendea lengo la kuumbwa kwao.Qur’an(102:8)
- Wabainike ni akina nani waliofuata njia sahihi ya maisha.-waislamu au makafiri.(Qur’an 16:39).
Uthibitisho wa kihistoria katika Qur’an kuwa ufufuo ni jambo jepesi mbele ya Allah(s.w).
- Mtu na punda wake waliokufa na kufufuka baada ya miaka mia(100).Qur’an(2:259).
- Kufufuka ndege wane(4) wa Nabii Ibrahim(a.s)-Qur’an(2:260).
- Kuamka kwa vijana wa pangoni baada ya kulala kwa miaka 309-Qur’an(18:25).
- Kufufuka kwa watu wa Nabii Mussa(a.s) waliokufa baada ya kutaka kumuona Allah(s.w) kwa jahara.Qur’an(2:55-56).
- Kufufuka kwa Yule mtu aliyeuliwa kwa dhulma.Alifufuka baada ya kupigwa na sehemu ya nyama ya ngo’mbe.Qur’an(2:72-73).
- Nabii Issa(a.s) kufufua wafu kwa idhini ya Allah(s.w).Qur’an(3:49).
Ushahidi wa ufufuo kutokana na maisha ya kila siku
- Kufufuka kwa ardhi wakati wa msimu wa mvua baada ya kufa kwake wakati wa msimu wa kiangazi.Qur’an(41:39).
- Kufufuka kutoka usingizini.Qur’an(30:23).
- Kufufuka kutoka kwenye kuzimia.
Maana halisi ya kuamini siku ya malipo
- Muumini ataendesha maisha yake kwa uadilifu hivyo ataepuka kufanya dhulma, unyonyaji na ukandamizaji.
- Muumini atatumia vipaji vyake vizuri katika kumuabudu Allah (s.w) akiwa na yakini kuwa ataulizwa juu ya vipaji alivyopewa.
- Muumini atajiepusha kufanya matendo maovu ili aepuke adhabu ya Allah (s.w).
- Muumini atafanya jitihada za kuyaendea matendo mazuri ili alipwe na Allah (s.w) pepo.
- Muumini ataleta istighfari na dua kumuomba Allah (s.w) amuepushe na adhabu ya moto.
- Muumini ataleta toba ya kweli atakapoteleza na kumuasi Mola wake.
Masharti ya toba
- Kufanya kwa ujinga au kutelezeshwa na wasiwasi wa shaitwani.
- Kujuta na kuilaumu nafsi.
- Kuazimia moyoni kuacha maovu.
- Iwapo makosa yanahusiana na kudhulumu haki za watu, waombwe radhi na kuwarejeshea haki zao.
- Kuzidisha kufanya vitendo vizuri mfano kutoa sadaka, kuleta funga za sunnah na swala za sunnah.
Toa ufafanuzi juu ya nini maana ya”shufaa” na ninani watakaostahiki shufaa.
(i) Shufaa ni uombezi wa watu wema kuwaombea msamaha watu watakaokuwa katika hali ya udhalili katika maisha ya akhera.
(ii) Watakaostahiki shufaa
- Wenye hisabu nzito
- Waja wema waingie peponi moja kwa moja bila ya hisabu.
- Wale ambao mizani ya mema na mabaya imekuwa sawa sawa waingizwe peponi.
- Watu wa motoni waingie-waingie peponi.
- Watu wema wapandishwe daraja katika peponi.
Nani watakao shufaia?
- Malaika.
- Mitume/Manabii.
- Watu wema.Mfano, mashahidi na watoto wachanga.
- Amali au vitendo vyema.
Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu.
Maana ya Qadar
Qadar ni kipimo au makadirio au kiasi.(54:49), (25:2) na (36:39).
Kukadiria kipimo maalumu.
Qadar ni mpango au utaratibu wa mfumo mzima unaomiliki kupatikana, kuwepo na hatimaye kutoweka viumbe vyote vilivyohai na visivyohai mbinguni na ardhini.(57:22) na (6:59).
Maana ya Qudra
Qudra ni uwezo wa Allah (s.w) juu ya kilakitu.
Qudra ni uwezo.
Qudra ni Uwezo wa Allah (s.w) usio na mipaka.(36:82), (54:50) na (7:54).
Umuhimu wa kuamini Qadar
- Ni nguzo ya sita ya imani ya kiislamu.
- Ni amri ya Allah (s.w) kuamini Qadar.
- Mwenye kukanusha nguzo hii hatabakia kuwa muislamu wa kweli bali atakuwa muongo.
Mtazamo wa Uislamu juu ya Qadar
Ni makosa makubwa kudhani kuwa mtu anaweza kufanya jambo lolote lile kinyume na Qadar ya Allah (s.w).
Ni makosa makubwa pia mtu kumlaumu Allah (s.w) kwa maovu anayoyatenda kuwa ndiye aliyemkadiria kufanya hivyo.
Uislamu umegawanya maisha katika maeneo haya mawili:
(i) Eneo ambalo mwanadamu hana uhuru/hiari nalo.
- Kuchagua wazazi wa kumzaa, kuchagua tarehe ya kuzaliwa na kufa, kuchagua rangi ya ngozi yake , kuchagua nchi na kuchagua kabila lake.
(ii)Eneo ambalo mwanadamu ana uhuru/hiari.
- Kumuasi au kumshukuru Allah (s.w).
- Kuua au kuacha viumbe hai.
- Uhuru wa kuwasaidia wasiojiweza kama chakula au kudhulumu.
- Kutoa haki za watu au kuzipokonya.
Allah (s.w) alimtunukia mwanadamu mambo haya ili aweze kuutumia uhuru wake vizuri;
- Utambuzibinafsi.
- Elimu.
- Vitabu vitukufu (Qur’an).
- Mitume (Manabii).
Pamoja na binadamu kuwa na uhuru wa kufanya alitakalo, isidhaniwe kuwa Allah (s.w) hajui kitakachotokea mpaka kitokee.
Allah (s.w) anayajua yote atakayoyafanya mja hadi hatima yake ya mwisho siku ya kiyama hata kablamtu huyo hajazaliwa.(11:6).
Isidhaniwe kuwa maadamu mtu amechagua kumuasi Allah (s.w), basi Allah (s.w) hana uwezo wa kumzuia, la hasha, kama ovu hilo halisadifu Qadar ya Allah (s.w), hataweza kulifanya.
Maana ya kuamini Qadar ya Allah(s.w) katika mchakato wa maisha ya kila siku.
- Muumini kwa kujua kuwa fursa,bahati,vipaji na neema mbalimbali alizonazo,amekadiriwa na Allah(s.w) hanabudi kuvitumia hivi kama aliyokabidhiwa ili kufikia lengo la kuumbwa kwake.
- Akijua pia kuwa neema zote alizonazo ni amana,hatalalama akipewa kichache bali ataridhia kuwa uchache wa neema alizonazo ndio makadirio ya Allah(s.w) na atamshukuru Allah(s.w) kuwa amemkadiria amana anayoweza kuitunza.
- Atajitahidi kutumia neema zote alizotunukiwa kwa kadiri ya uwezo wake,kasha matunda ya jitihada hizo atayategemeza kwa Allah(s.w).
- Anapotokewa na misukosuko mbalimbali iliyo nje ya uwezo na jitihada za kibinadamu huwa ni mwenyekutulizana na kusubiri.Qur’an(57:22-23),(2:155-156).
- Huwa jasiri katika kupigania haki na kusimamisha uislamu katika jamii kwa kumtegemea Allah(s.w) ambaye ndiye mdhibiti wa kila jambo.
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA DINI.
Makundi makuu ya Dini yaliyotajwa katika Qur’an.
Aina za dini (64:2)
- Dini ya Allah (s.w)-Uislamu (3:83) na (3:19).
- Dini za watu-Ukafiri, Ushirikina na Utawa.
Tofauti zilizopo kati ya Uislamu na dini nyingine za watu
Tofauti hizi zitazingatia maana, Itikadi na Madhara au Matunda ya dini husika.
- Dini ya Ukafiri
Neno kafiri limetokana na neno “Kufr” lenye maana ya kukana au kufunika ukweli uliodhahiri.
Dini ya ukafiri ni njia ya maisha iliyofumwa na mwanadamu kwa msingi wa kukana ukweli wa kuwepo Allah (s.w) Muumba pamoja na kuukana mwongozo wake aliomshushia mwanadamu.Qur’an (5:44).
Vipengele vya Itikadi ya Ukafiri
- Hakuna Muumbawa Ulimwengu na vyote vilivyomo.Bali ulimwengu pamoja na mwanadamu,vimeibuka vyenyewe kwa bahati(chance creation) nasibu.
- Hapana kusudio au lengo lolote la maumbile.
- Kwa kuwa hakuna Muumba wa ulimwengu,mwanadamu anajukumu la kuunda utaratibu wa maisha atakaoufuata ili kumuwezesha kuishi kwa furaha na amani.
- Hapana maisha mengine baada ya maisha haya ya hapa ulimwenguni.Kwa kuwa ulimwengu na mwanadamu vimetokea kwa bahati nasibu,hivyo vitatoweka hivyohivyo kama vilivyozuka.
Madhara ya itikadi ya ukafiri katika jamii.
- Kukosekana kwa wema na huduma ya bure.Masikini na wanyonge hawapati misaada na huduma kutoka kwa matajiri kwa kuwa hawana cha kulipa.
- Masikini na wanyonge hukandamizwa na kudhulumiwa haki zao matajiri na wenye hadhi.
- Kushamiri na kuenea kwa vita ulimwenguni ni matunda ya ukafiri.
- Kuenea kwa zinaa katika jamii.
- Kuporomoka kwa maadili katika jamii.Haya na utu kutoweka.
- Kuenea kwa ulevi,madawa ya kulevya,kamari na rushwa.
- Watetezi wa haki hukamatwa na kuadhibiwa na kupachikwa majina mabaya mabaya kama vile wapinga maendeleo,vibaraka wa maadui,magaidi na wachochezi.
2. Dini ya Ushirikina
Ni mfumo wa maisha uliobuniwa na mwanadamu uliojengwa juu ya itikadi ya kuwepo miungu wenye ushirika na Mwenyezi Mungu (s.w).
Miungu hawa walioshirikishwa na Mwenyezi Mungu (s.w) wamepachikwa uwezo wa kumiliki na kuyaendesha maisha ya mwanadamu ya hapa ulimwenguni.
Madhara ya dini ya Ushirikina
- Kumfanya mwanaadamu aamini na kufuata mambo kibubusa.
- Huwafanya watu waishi katika maovu kwa tama ya kupata shufaa mbele ya Alla (s.w) kupitia kwa waungu wanaoshirikishwa naye.
- Kuenea kwa vifu vya watu wasio na hatia.
3.Dini ya Utawa
Utawa ni hali ya kujitenga na shughuli za dunia au kujiweka katika hali ya kujinyima raha za kimwili na kujiepusha na maudhi ya walimwengu.
Ni dini ya kujitenga na shughuli pamoja na maudhi ya walimwengu ili kupata wasaa wa kumtumikia Mwenyezi Mungu (s.w) na kupata radhi zake kwa urahisi.
Itikadi ya Utawa
- Kuna Muumba mmoja wa ulimwengu na vyote vilivyomo.
- Lengo la maisha ya mwanadamu ni kumtumikia Mwenyezi Mungu (s.w) ili kupata maisha ya furaha ya milele huko Akhera.
- Kujitenga na maisha ya dunia kwani kuishi kwa raha duniani ni ishara ya kukosa maisha ya raha huko Akhera.Qur’an (57:26-27).
Madhara ya Utawa
- Utawa unawatoa watu wazuri na wanyenyekevu katika jamii kwenye shughuli muhimu za maisha na kuwafanya w aishi maisha ya kivivu ya kujitenga na dunia.
- Kugawa matendo ya dini na dunia jambo ambalo linapelekea watu waovu waongoze jamii na wanadamu kuwa katika tabu za kila namna.
- Watawa hufanywa ni wacha-Mungu na wanapokufa au hata wakiwa hai hupachikwa sifa za Mwenyezi Mungu (s.w) kitendo ambacho ni cha ushirikina.Huidumbukiza jamii katika ushirikina.
4.Dini ya Uislamu
Itikadi ya Uislamu
Uislamu ni Dini ya Allah (s.w) iliyojengwa juu ya Itikadi zifuatazo:
- Muumba na mmiliki wa ulimwengu na vyote vilivyomo ni Mwenyezi Mungu,Mwenye uwezo,Ujuzi na Hekima juu ya kila kitu.
- Mwenyezi Mungu amemuumba mwanadamu ili amuabudu yeye pekee kwa kumtii na kumnyenyekea katika yake yote.
- Viumbe vyote vilivyomzunguka mwanadamu katika ulimwengu viko pale kwa ajili ya maisha yake.
- Mwanadamu hapa ulimwenguni ni khalifa wa Mwenyezi Mungu mwenye dhima ya kusimamisha ufalme wake kwa kufuata mwongozo wake aliowashushia wanadamu kupitia kwa mitume na vitabu vyake.
- Pana maisha ya Akhera.Watu wema walipwe pepo na waliofanya maovu walipwe moto.
Matunda ya kusimama kwa Uislamu katika jamii
- Humkomboa mwanadamu kutokana na utumwa wa aina zote.
- Humfanya mwanadamu awe muadilifu katika utendaji wa maisha ya kila siku.
- Humfanya mwanadamu awe mpole na mwenye huruma kwa mwanadamu wenziwe na viumbe wengine.
- Humfanya mwanadamu awe mvumilivu na mwenye subira.
- Humfanya mwanadamu awe mwenye kukinai
- Huwawezesha wanadamu kusimamisha haki na kuleta usawa katika jamii.
- Humuwezesha mwanadamu kuwa na mtazamo mpana na sahihi juu ya maisha.
- Humfanya mwanadamu awe jasiri katika kusimamisha haki katika jamii.
3.CHIMBIKO LA FIQH
Mgawanyiko wa madhehebu
Sababu zilizopelekea kutokea madhehebu
Katika kipindi cha Tabiina Dola ya Kiislamu ilikuwa imepanuka sana hivyo yaliiibuka matatizo yaliyohitajia ufafanuzi wa kisheria.Ili kuepusha jamii kuchanganya sheria, kanuni za Uislamu na mila za jamii ilihitajika Fat-wa.
Sababu zilizopelekea kutolewa Fat-wa mbalimbali ni hizi:
(i) Kuibuka kwa matatizo ya kisheria, taratibu za kibiashara na uchumi.
(ii) Mila na desturi za watu mbalimbali ziliibuka na kutishia kufanywa sehemu ya mafunzo ya Uislamu.
Maimamu wafuatao walisimama imara na kutoa Fat-wa juu ya masuala mbalimbali kulingana na Qur’an na Sunnah.
(i) Imam Nu’man bin Thabit Abu Hanifa: Ananasibishwa na madhehebu ya Hanafy.
(ii) Imam Malik bin Anas: Ananasibishwa na madhehebu ya Maliky.
(iii) Imam Muhammad bin Idrisa Al-Sahafii: Ananasibishwa na madhehebu ya Shafiiy.
(iv) Imam Abu ‘Abdallah Ahmad bin Muhammad bin Hambal: Ananasibishwa na madhehebu ya
Hambaliy.
Maimamu hawakuwagawa waislamu katika madhehebu bali waliwaunganisha waislamu na waliheshimiana sana na walikuwa ni wacha Mungu na wafuasi halisi wa Uislamu.
Baada ya kutawafu maimamu hawa, wafuasi wa fat-wa zao walianza kujinasibisha na madhehebu ya maimamu hawa, ijapokuwa haisemwi zipo hisia kwa kila wafuasi wa maimamu hawa kuwaona wengine hawako sawa na kutoa mwanya wa kuwagawa waislamu.
Waasisi wa madhehebu ni maadui wa Uislamu ili kuuhilikisha Uislamu kwa kuwafanya Waislamu washughulike na migogoro ya wao kwa wao na wasiihangaikie Dini yao.Madhehebu kama Salafy, Qadiriyah na Shi’ah ni miongoni mwa na zao la mikakati ya maadui ya kuusambaratisha Uislamu.
Msimamo wa Uislamu juu ya madhehebu
Madhehebu katika Uislamu ni uzushi kutokana na sababu zifuatazo:
- Mtume (s.a.w) hakuwa na dhehebu bali alikuwa ni Muislamu.
- Allah (s.w) ametusisitiza tufuate mila ya Ibrahim (a.s) ambayo ni Uislamu na si madhehebu.
- Madhehebu yanawagawa Waislamu hivyo yanapelekea nguvu ya Uislamu kudhoofika na kuporomoka.
- Hakuna aya wala hadithi sahihi inayosisitiza kuwa waislamu washikamane na madhehebu na waache maelekezo ya Allah (s.w) na Mtume wake.
- Allah (s.w) amekemea vikali suala la waislamu kugawanyika na akaonesha ni moja ya sababu za kuuacha Uislamu na kuwa washirikina. (30:30-31).
- Mtume (s.a.w) amesisitiza kuwa yeyote yule atakaye kuja kuwafarakanisha waislamu ni halali kukatwa kichwa, hivyo madhehebu kama yanavyo nadiwa yanawafarakanisha waislamu.
FAMILIA YA KIISLAMU
Ndoa katika Uislamu.
Maana ya ndoa
- Ni mkataba wa hiari wa kuishi pamoja kati ya mwanaume na mwanamke kwa kufuata utaratibu uliowekwa na jamii.
Ndoa ya kiislamu
- Ni mkataba wa hiari wa kuishi pamoja kati ya mume na mke kwa kufuata taratibu na sheria za kiislamu.
Umuhimu wa ndoa katika Uislamu
- Kuihifadhi jamii na zinaa.(4:24) na (5:5).
- Kuendeleza kizazi kwa utaratibu mzuri.(42:11) na (4:1).
- Kujenga mapenzi na huruma katika familia.(30:21) na (2:287).
- Kukuza uhusiano na udugu katika jamii.(25:54) na (49:13).
- Kulea kizazi katika maadili ya kiislamu.
- Kuwafanya watu wawajibike ipasavyo.(6:151)
Taratibu za kuoa Kiislamu
1.Kuchagua mchumba
Mambo ya kuzingatia wakati wa kuchagua mchumba:
- Dini.
- Tabia njema.
- Umaharimu.
- Sifa nyinginezo.
Pia wanawake wanaweza kuolewa kwa sifa hizi; mali, uzuri na nasaba.
Mtume (s.a.w) amesisitiza sana tuchague mchumba mwenye msimamo mzuri wa dini.
Sifa nyingine za kuchagua mchumba ni rika au umri, upendo na huruma na Elimu.
Umaharim
Maharimu ni wanawake na wanaume walioharamishwa kuoana kutokana na ukaribu wa nasaba.
Wanawake walioharamishwa kuwaoa ni hawa wafuatao:
- Mwanamke aliyepata kuolewa na baba yako.
- Mama aliyekuzaa.
- Binti yako uliye mzaa na binti wa kunyonya na mwanao.
- Dada yako khalisa au wa kwa baba au wa kwa mama.
- Shangazi yako.Dada wa baba yako.
- Mama mdogo-ndugu wa mama yako.
- Binti wa ndugu yako mwanamume khalisa au wa kwa baba au kwa mama.
- Binti wa dada yako khalisa au wa kwa baba au wa kwa mama.
- Mama wa kukunyonyesha.
- Dada yako wa kunyonya naye.
- Mama yake mkeo wa kumzaa au wa kumnyonyesha.
- Binti wa mkeo uliyemuingilia.
- Mke aliyeolewa na mwanao wa kumzaa au wa kumnyonyeshwa na mkeo.
- Mtu na ndugu yake pamoja (au) mtu na shangazi yake au mtu na mama yake mdogo pamoja.
- Mke wa mtu.
Mahari
Ni zawadi au hidaya anayopewa mwanamke anayeolewa kwa Amri ya Allah (s.w) na Yule mwanamume anayemuoa.
Mahari hayana kiwango maalumu na ni uhuru wa mwanamke anayeolewakutoza mahari kiasi apendacho.Qur’an (4:24).
2.Kufunga ndoa ya Kiislamu
Ili ndoa ya kiislamu ifungwe ni lazima yatekelezwe yafuatayo:
(i) Mume atekeleze masharti ya kuoa
- Aoe kwa hiari yake.
- Asiwe maharimu wa mke anaye muoa.
- Anaye muoa awe muislamu.
- Awe baleghe na mwenye akili timamu.
- Asiwe katika Ihramu ya Hija.
- Asiwe na ndoa ya wake wanne ambao anaishi nao katika ndoa.
(ii) Mke atekeleze masharti ya kuolewa
- Asiwe katika ndoa ya mtu mwingine.
- Asiwe katika eda ya mume mwingine.
- Awe mwema.
- Asiwe maharimu kwa mume anaye muoa.
- Awe na akili timamu.
- Asiwe katika Ihramu ya Hija.
(iii) Pawe na walii au Idhini yake
Walii ni muozeshaji au mfungisha ndoa.
Walii ni hawa kwa daraja zao:
- Baba mzazi wa mwanamke anayeolewa.
- Babu mzaa baba yake.
- Ndugu yake wa kiume wa baba mmoja na mama mmoja.
- Ndugu yake wa kiume wa baba mmoja.
- Mtoto wa kiume wa ndugu yake wa kiume wa baba mmoja na mama mmoja.
- Baba yake mdogo aliyezaliwa na baba yake wa kwa baba mmoja na mama mmoja.
- Baba yake mdogo aliyezaliwa na baba yake wa kwa baba tu.
- Mtoto wa kiume wa baba yake mdogo wa kwa baba yake mdogo na mama.
- Mtoto wa kiume wa baba yake mdogo kwa baba tu.
- Serikali (Hakimu au Kadhi) katika nchi za kiislamu.
(iv) Pawe na mashahidi wawili
Zifuatazo ni sifa zao:
- Wawe wtu wazima waliokwisha baleghe.
- Wawe na akili timamu.
- Wawe waislamu wanaume.
- Wawe waadilifu.
- Wawe waungwana (sio watumwa).
(v) Ridhaa (Idhini) ya mwenye kuolewa
(vi) Pawe na Ijabu na Kabuli
Ijabu:Ni maneno anayosema walii kumwambia mume anayeoa:
“Nimekuoza Aisha bint Mfaume”
Kabuli:Ni maneno ya kukubali kuoa:
“Nimemuoa Aisha bint Mfaume”
Mtazamo wa Qur’an juu ya kuoa mke zaidi ya mmoja
Allah (s.w) ameruhusu waislamu waoe wake hadi wane.Qur’an (4:3).
Mafunzo tunayoyapata kutoka katika Qur’an (4:3)
- Uke wenza ni ruhusa kutoka kwa Allah (s.w) hivyo wanaume wema na wanawake wema wa kiislamu hawanabudi kuipokea ruhusa hii kwa lengo la kumcha Allah (s.w).
- Ruhusa hii ni kuoa wake hadi wane (4) tu na sio zaidi.
- Ruhusa hii imetolewa ili kuwaruhusu wanaume wema wa kiislamu wawoe wajane au wanawake wema wanaohitajia hifadhi hiyo ya kimwili au kuepusha wanawake wema kuolewa na wanaume waovu.
- Endapo mwanaume hatakuw na uwezo wa kukidhi matamanio ya jimai kwa wake zake wote au hatakuwa muadilifu kwa wake zake wote,basi sheria hii inamnyima kuoa mke zaidi ya mmoja.
- Hapana mwanamke anayelazimishwa kuolewa na mume mwenye mke.
Hekima ya kuoa wake hadi wane (4)
- Kurahisisha ulezi wa watoto yatima.
- Kuwahifadhi wanawake wajane na walioachika.
- Kuwapa hifadhi wanawake waliozidi idadi ya wanaume.
- Kuwapa fursa wanaume ya kupata watoto iwape wake zao wa mwanzo ni tasa.
- Kumpa mwanaume msaada na maliwazo endapo mke wa kwanza atakuwa amepata maradhi ya kudumu kiasi cha kumfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake kwa mumewe
Majukumu katika familia
1 Wajibu wa mume kwa mkewe
- Kumlisha, kumvisha na kumpatia makazi kwa kadri ya uwezo wake.(65:7).
- Kumtendea wema, kumhurumia na kumpenda.Qur’an (4:19).
- Kujizuia kumchukia mkewe.
- Kujizuia kumpiga au kuwa mkali sana kwake.(4:34).Kumpiga kwa nguo au mti wa mswaki.
- Kutunza siri za nyumba.
- Kuwa muadilifu.
- Kusimamia maadili ya kiislamu na Ucha Mungu.
2. Wajibu wa mke kwa mumewe
- Kumtii mumewe katika mambo yote mema atakayomuelekeza.(2:228) na (4:34).
- Kumfurahisha mumewe na kumliwaza.
- Kuhifadhi nyumba na mali ya mumewe.
- Kuwa na subira juu ya mumewe.(42:43).
- Kutosheka na kile anachopewa na mumewe.(65:7) na (33:28-29).
- Kumuusia mumewe na kumkumbusha kumcha Allah (s.w).
3.Wajibu wa wazazi kwa watoto
- Kuwalea kimwili kwa kuwalisha,kuwavisha na kuwapa makazi mazuri kwa kadri ya wasaa.
- Kuwalea kimaadili.Kuwaelimisha katika mfumo wa elimu wa kiislamu na kuwafundisha maadili ya kiislamu kinadharia na kimatendo.
- Kuwapenda na kuwahurumia kwa kuchunga mipaka ya Allah(s.w).(9:23-24) na (58:22).
- Kuwaombea dua watoto wawe wacha Mungu.(25:74).
- Kuwanasihi.(2:132-133) na (31:13-19).
4.Wajibu wa watoto kwa wazazi
- Kuwatii wazazi katika yale yote yanayowafikiana na sheria za Allah (s.w).
- Kuwaheshimu wazazi na kuongea nao kwa upole na huruma na kujizuia kubishana nao.
- Kuwahurumia wazazi na kuwapa msaada wowote wanaotarajia kwa kadri ya uwezo alimradi tu izingatiwe mipaka ya Allah (s.w).
- Kuwausia wazazi kumcha Allah (s.w) na kuwaombea dua na maghfira.Qur’an (14:41) na (46:15).
5.Wajibu wa watumishi katika familia
- Kuwatendea wema kama ndugu zetu.
- Tuwalipe kama tulivyopatana kabla ya jasho lao halijakauka.
- Tuwahurumie na tukiwapa kazi ngumu tuwasaidie.
- Kuwalisha, kuwavisha na kuwapa makazi sawa nay ale tunayowapa watoto wetu.
- Tuwasamehe wanapokosa na tujiepushe kuwafanyia ukatili wa aina yoyote.
6.Wajibu kwa mayatima
- Kuwatendea wema kama tufanyavyo kwa watoto wetu.
- Kutokuwanyanyasa yatima.(107:1-2).
- Kuwatunzia mali zao kwa uadilifu.(4:10).
7.Wajibu wa wadogo kwa wakubwa
- Kuwatii na kuwaheshimu wakubwa zao.
8.Wajibu wa wakubwa kwa wadogo
- Kuwaheshimu na kuwahurumia.(53:32) na (49:13).
Kudhibiti uzazi katika Uislamu
Nadharia juu ya kampeni ya kikafiri ya kudhibiti uzazi na madhara yake
Ni ipi maana ya kudhibiti uzazi?
Ni njia za kuzuia mimba kwa kumtumia mwanaume au mwanamke ikiwa ni pamoja na kutoa mimba (Abortion) na kuviza kizazi (sterilization).
Sababu zilizopelekea kustawi kwa kampeni ya kudhibiti uzazi
- Matokeo ya mapinduzi ya viwanda (Industrial Revolution) ya huko Ulaya.Kuhitajika kwa maelfu ya wafanya kazi.
- Pato la mfanyakazi halikumuwezesha kuihudumia familiayake, mke na watoto pia walilazimika kufanya kazi viwandani ili kupata riziki zao.Kuzaa kukawa ni nuksi.
- Mapinduzi hayo yaliambatana na utamaduni wake.Utamaduni ulihimiza maendeleo na ustawi wa mtu binafsi.Kuwa na vitu vingi vya anasa na fahari.
- Kuparaganyika kwa familia kukapelekea kuondoka kwa uadilifu wa ndoa.
Hoja wanazotoa wapiga debe wa kampeni ya kudhibiti uzazi
1.Watu wanaongezeka kwa kasi kuliko rasilimali, hivyo itafikia wakati rasilimali zitakwisha na watu kufa.
Udhaifu
(i) Rasilimali zote ambazo mwanadamu anazihitaji zilikuwepo tokea dunia ilipoumbwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu wa zama zote.Rasilimali hutambulika kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.
(ii) Historia hivi sasa inaonesha kuwa kuongezeka kwa watu hakusababishi uhaba wa mahitaji muhimu.Mfano, 1880 idadi ya wajerumani ilikuwa milioni 45 wakati huo kulikuwa na uhaba wa chakula ukilinganisha na hivi sasa ambapo idadi yao ni zaidi ya milioni 68.
(iii) Allah (s.w) anadhibiti uwiano wa viumbe walioko ulimwenguni kulingana na rasilimali zilizopo.Mfano, samaki “Starfish” hutaga mayai miambili milioni kwa mara moja,kama yote yataanguliwa baada ya vizazi vichache tu samaki huyo atazijaza bahari za dunia nzima na isiwepo hata nafasi ya tone la moja la maji.
(iv) Tatizo ni kasoro za kibiashara, ugawaji na usambazaji wa rasilimali.
2.Tatizo la vifo na maradhi.
Husababisha machungu na mateso ya kimwili na kisaikolojia.
Binadamu atafute njia nzuri ya kujipunguza (kudhibiti uzazi) badala ya kungojea majanga kama njaa au mafuriko.
Udhaifu
(i) Uhai na kifo havipo katika miliki ya binadamu.Hadhari yoyote itakayochukuliwa, kifo lazima kitokee.
(ii) Ni hadhari gani ambayo binadamu anaweza kuichukua dhidi ya tetemeko la ardhi, kimbunga na maradhi mabaya?
3.Watu masikini wasizae watoto wengi ili waweze kutosheleza mahitaji ya watoto wachache walionao.(Ugumu wa malezi).
Kuwapa elimu nzuri na kuwalea katika hali nzuri kimaisha.
Udhaifu
(i) Ni hatari kwa ustawawi wa Taifa ikiwa kizazi cha binadamu kitalelewa katika starehe na anasa ya mali waliyoichuma na iwapo hawatakabiliwa na matatizo na misukosuko ya maisha.
Hivyo uvumilivu, subira, ukakamavu na ujasiri ni mambo yatakayoijenga tabia ya binadamu na kumfanya awe mtu mwenye manufaa katika jamii.
(ii) Ni kosa kuacha kutazama hali ya binadamu na mazingira yake na kuangalia hali ya maisha ya mahali pengine na hivyo kuanza jitihada na kujaribu kuwakuta waliotangulia.
“Elimu bora” na “Hali bora ya maisha” ni misemo tata isiyo na tafsiri moja maalumu.
4.Kwa watu masikini ni bora kutozaa kuliko kuzaa watoto watakaokufa kwa utapiamlo na maradhi.
Udhaifu
(i) Kila kiumbe kilichoumbwa na Allah (s.w) amekikadiria riziki yake.
(ii) Maradhi kwa binadamu hayaepukiki na hayachagui masikini tu bali hata tajiri.
5.Kuzaa watoto wengi kunaharibu afya ya mama.Umbo na sura huathiriwa.
Udhaifu
(i) Njia zinazotumiwa kuzuia mimba pia zina madhara kwa afya ya mama.Wanawake wengi wameathiriwa na maradhi mbalimbali na hata kupoteza maisha kutokana na athari ya madawa hayo.
(ii) Kwa hoja za Afya(Medical resons) mtu hawezi kuweka sheria mwanamke azae watoto idadi kadhaa (wangapi).Jambo hili linategemea tofauti iliyopo kati ya mwanamke mmoja na mwingine.
Mtazamo wa Uislamu juu ya kudhibiti uzazi.
- Kuhusu riziki , Allah (s.w) hakuumba kiume chochote ila amekikadiria riziki yake.
- Umaskini hauletwi na kuzaana kwa wingi bali husababishwa na mifumo ya maisha ya kitwaghuti iliyo dhidi ya mfumo sahihi wa Allah (s.w).
- Ubora wa binadamu haupatikani kwa kuhodhi rasilimali nyingi, bali hupatikana kwa kujipamba na maadili mema anayoridhia Allah (s.w).
- Kudhibiti uzazi katika Uislamu kunaruhusiwa katika dhana ya kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Sababu zinanazopelekea Uislamu kupinga kampeni za kudhibiti uzazi.
- Dhana kuwa wanadamu wakiwa wengi watakosa riziki ni potofu ambayo imejengwa juu ya msingi wa ukafiri ambao unamfumo wa maisha unaonyonya, kukandamiza na kudhulumu haki za watu.
- Matatizo ya uchumi yameshawekewa ufumbuzi wake katika mfumo wa kiislamu.
- Sera ya kudhibiti uzazi inachochea zinaa.
- Kuweka sera ya kudhibiti uzazi ni kuingilia utaratibu(mamlaka) ya Allah(s.w) ambaye ameweka utaratibu wa mahusiano ya mwanamume na mwanamke yawe kwa njia ya ndoa na malengo ya ndoa ni kuendeleza kizazi cha binadamu kwa njia nzuri.
- Uislamu unapinga kampeni za kudhibiti uzazi kama sera ya kitaifa na kimataifa na inakubali kwa mtu mmoja mmoja kulingana na hali na mazingira yake.
- Njia zitumikazo kuzuia uzazi zinamadhara(side effects).
Sababu zinazokubalika za kudhibiti uzazi
- Kuhifadhi au kulinda afya ya mama.
- Iwapo mwanamke yungali ananyonyesha mtoto mchanga.
Talakana Eda
Maana ya talaka
- Ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa baina ya mume na mke mbele ya mashahidi wawili kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa katika sheria ya kiislamu.
Talaka katika Uislamu si jambo linalopendeza bali linaruhusiwa tu pale inapokuwa hapana budi.
Talaja inabidi pale itakapoonekana kuwa lengo la ndoa halifikiwi tena.
Hekima ya kuruhusiwa talaka
- Ni kuwapa wawili wanaoachana fursa nyingine ya kuanzisha maisha mengine ya familia na kuyaendeleza kwa lengo tarajiwa.
Taratibu za suluhu kati ya mume na mke
Mume namke wanapogombana kabla ya kufikia hatua ya talaka, inatakiwa ifanyike suluhu kwa kufuata utaratibu ufuatao:
(i) Mume na mke, wafanye subira kwa kujisuluhisha kwa kutakana radhi na kusameheana.Qur’an (24:22), (42:40) na (41:28).
(ii) Mume au mke anaruhusiwa kujitenga na mwenzake kwa kipindi kisichozidi miezi mine (4).Qur’an (2:226-227).
(iii) Jamaa wa pande mbili wa mume na mke wawkutanishe na kuwasuluhisha.Qur’an (4:35).
Mwanamke anaruhusiwa kuomba talaka katika mazingira haya:
Pale atakapoona kuwa mumewe hamtendei haki na malengo ya ndoa hayafikiwi.
Kama tangu mwanzo katika kufunga mkataba wa ndoa,mume alikubaliana na mumewe kuwa atakuwa na uhuru wa kuvunja ndoa endapo atamfanyia jamboa asilolipenda na lililo kinyume na sheria.
Kama katika mkataba wa ndoa mwanaume alitoa haki ya kutamka talaka na kumpa mkewe ili kumpa uhuru na uwezo zaidi wa kuvunja mkataba wa ndoa.
Aina za Talaka
Kuna aina kuu mbili za talaka ambazo ni:
- Talaka rejea
- Talaka isiyo rejea.
Talaka rejea
Ni aina zote za talaka zinazompa mtu fursa ya kumrejea mkewe baada ya kumpa talaka.
Ifuatayo ni migawanyo yake:
(i) Talaka moja
Hupatikana baada ya kumtamkia mke “nimekuacha” kwa talaka moja katika kipindi muafaka mbele ya mashahidi wawili.
(ii) Talaka mbili
Hupatikana baada ya kumuacha mke kwa talaka moja kisha ukamrudia na ukamuacha tena kwa talaka moja nyingine.AU
Hupatikana kwa kumuacha mke kwa talaka mbili katika twahara mbili tofauti katika kipindi cha eda.Qur’an (2:229).
(iii) Talaka ya Zihar
Inapatikana kwa mume kumsusa mkewe kwa kumfananisha na mama yake au maharimu wake.Kama hatatekeleza masharti yaliyoainishwa katika Qur’an (58:3-4) kabla ya miezi mine kuisha, mkewe atakuwa ameachika.
(iv)Talaka ya khula
Inapatikana kwa mke kudai talaka au kumtaliki mumewe kutokana na makubaliano waliyoweka tangu awali katika mkataba wa ndoa.
Mke aliyedai talaka atalazimika kumrudishia mumewe mahari aliyompa ili ajikomboe.Qur’an (2:229).
(v)Talaka ya Mubarat
Inapatikana kwa mume na mke kukubaliana kuachana kwa wema baada ya kuona kuwa hawafikii malengo ya ndoa.
(vi)Talaka kabla ya jimai
Kuvunja ndoa kabla ya tendo la ndoa.
Utaratibu wake ni huu:
- Hapana kukaa eda kwa mwanamke aliye achwa.
- Kama mume ameshatoa mahari hatodai chochote kama ndiye aliyemuacha mkewe.
- Mume atalazimika kumpa mkewe kitoka nyumba kama ndiye aliyeamua kumuacha.
- Ikiwa hajatoa mahari atalazimika kutoa nusu mahari waliyokubaliana.
- Kama mke ndiye aliyedai talaka atamrudishia mumewe mahari aliyompa.Qur’an (2:236-237).
Talaka isiyo rejea
Ni aina zote za talaka ambazo hazimpi mtu fursa ya kumrejea mkewe baada ya kuachana mpaka aolewe na mume mwingine, kasha akiachika ndio anaweza kumuoa tena.
Migawanyo ya aina hii ya talaka:
(i) Talaka tatu
Hupatikana kwa kumuacha mke kwa talaka tatu kwa kumtamkia katika kila kipindi cha twahara katika kipindi cha eda.
AU
Hupatikana kwa kumuacha mke aliye rejewa baada ya kutoa talaka mbili.
Hairuhusiwi kutoa talaka tatu mfululizo katika twahara ya kwanza ya kipindi cha eda.
(ii) Talaka ya Li’aan
Hupatikana baada ya mume au mke kumshika ugoni mwenzake bila ya kuwa na mashahidi wane, ikabidi kila mmoja kuishuhudisha nafsi yake kwa kula kiapo mbele ya kadhi.Qur’an (24:6-9).
Taratibu za kutaliki Kiislamu
Rejea Qur’an (65:1-6) na (2:228-229).
- Talaka hutolewa kwa matamshi au maandishi kuwa nimekuacha.
- Utoaji wa talaka ushuhudiwe na mashahidi wawili waadilifu.
- Talaka itamkwe /itolewe wakati mke akiwa katika kipindi cha twahara (asiwe katika hedhi na nifasi) na wasiwe wamefanya tendo la ndoa katika kipindi hicho.
- .Baada ya talaka kutolewa mke analazimika kukaa eda katika nyumba ile ile aliyokuwa akiishi na mumewe.
- .Kama wawili hawa wataamua kureana kabla ya eda kwisha watarejeana kwa wema kwa kumuahidi Allah (s.w) kuwa wataishi kwa wema.
- Baada ya eda wawili hawa wanaamrishwa na Allah (s.w) kuachana kwa wema.
- .Si halali kwa mwanaume anayetoa talaka kuchukua chochote katika vile alivyompa mkewe..
- .Mwanaume anayemuacha mkewe analazimika kumpa mtalaka wake kitoka nyumba.Qur’an (2:236).
- .Mwanamke aliyeomba talaka anawajibika kujikomboa kwa kumrudishia aliyekuwa mume wake mahari aliyompa.Mume akisamehe mahari hayo hapana lawama.
Eda
Eda ni kipindi cha kungojea mwanamke aliyeachwa au aliyefiwa na mumewe kabla hajaruhusiwa kuolewa na mume mwingine.
Eda ya kuachwa ni twahara tatu au miezi mitatu kwa wasiopata hedhi.
Eda ya mke mwenye mimba huishia atakapojifungua.
Eda ya mke aliyefiwa na mume ni miezi mine na siku kumi (10).
Hairuhusiwi kutoa talaka tatu mfululizo katika twahara ya kwanza ya kipindi cha eda.
Ni ipi hekima ya Eda?
- Kuwapa wawili muda wa kufikiri vizuri ili ikiwezekana wapatane tena.Qur’an (65:1).
- Kuthibisha uhalali wa mtoto wa mume wa mwanzo asijepewa mume atakayefuata.
Mirathi katika Uislamu
Ni ipi maana yaMirathi?
Mirathi ni kanuni na taratibu za kugawa mali aliyoiacha mtu aliyekufa kwa ndugu na jamaa wa karibu kwa mujibu wa sheria.
Mirathi ya kiislamu inafuata kanuni na taratibu alizoziweka Allah (s.w).
Uislamu unampa haki mwanamke ya kurithi kama ilivyo kwa wanaume.Qur’an (4:7).
Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawa urithi
1.Haki zinazofungamana na mali ya urithi
- Madeni
- Zakat kama haijatolewa
- Gharama za makazi ya mke katika kipindi cha eda au mwaka mzima atakapoamua kubakia.
- Usia ambao hauzidi theluthi (1/3) ya mali iliyoachwa.
2.Sharti za kurithi
- Kufa mwenye kurithiwa.
- Kuwepo hai mrithi wakati akifa mrithiwa.
- Kukosekana mambo yenye kumzuia mtu kurithi.
3.Mambo yanayomzuia mtu kurithi
- Kumuua amrithiye ijapokuwa kwa bahati mbaya.
- Kutofautiana katikadini.
- Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa hatamrithi baba aliye mzaa wala baba hatamrithi mtoto huyo.
4.Sababu za kurithi
- Kuwa na nasaba na marehemu.
- Kuwa katika ndoa ya halali na marehemu.
- Kuacha huru mtumwa.Mwenye kumpa uhuru mtumwa humrithi huru wake.
Kukokotoa hesabu za Mirathi
Mgawanyo wa mirathi kwa mujibu wa Qur’an (4:11-12).
“Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu; mwanamume apate sawa na sehemu ya wanawake wawili.Na ikiwa wanawake ni (wawili au) zaidi ya wawili, basi watapata thuluthi mbili ya mali aliyoiacha (maiti).Lakini akiwa mtoto mwanamke ni mmoja , basi apewe nusu. Na wazazi wake wawili kila mmoja wao apate sudusi (1/6) ya mali aliyoiacha (maiti), akiwa maiti huyo anaye mtoto au mjukuu.Lakini kama hana mtoto, na wazazi wake wawili wamekuwa ndio warithi wake basi mama yake atapata thuluthi moja (1/3) na (baba) thuluthi mbili (2/3). Na kaka huyo (maiti) anao ndugu, basi mama yake atapata sudusi moja (1/6). Na huku kurithi kunakuwa baada ya kutoa aliyoyausia au kulipa deni… ” (4:11).
“Na nyinyi mtapata nusu (1/2) ya (mali) walizoacha wake zenu, kama wao hawana watoto (wala wajukuu). Na ikiwa wana mtoto (au mjukuu), nyinyi mtapata robo (1/4) ya walivyoviacha, baada ya kutoa walivyousia au kulipa deni. Nao (wake zenu) watapata robo ya mlivyoviacha ikiwa hamna mtoto (wala mjukuu).Lakini ikiwa mnaye mtoto (au mjukuu), basi wao (hao wanawake) watapata thumni (1/8) ya vile mlivyoacha, baada ya kutoa mlivyousia au kulipa deni.Na kama mwanamume au mwanamke ni mkiwa-hana mtoto (walamjukuu) wala wazazi, lakini anaye kaka wa kwa mama au dada (wa kwa mama pia), basi kila mmoja katika hawa atapata sudusi (1/6).Na wakiwa zaidi kuliko hivyo, basi watashirikiana katika thuluthi (1/3). Baada ya kutoa vilivyousiwa au kulipa deni pasipo kuleta dhara.Huu ndio wasia uliotoka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mpole”.(4:12).
Wenye kurithi wanaume ni hawa:
1.Mtoto mwanaume.
2.Mtoto mwanamke wa mtoto mwanaume (mjukuu).
3.Baba.
4.Babu wa kwa baba.
5.Ndugu wanaume wa kwa baba na mama.
6.Ndugu mwanaume wa kwa baba tu.
7.Ndugu mwanaume wa kwa mama tu.
8.Mtoto mwanaume wa kwa ndugu mwanaume wa kwa baba na mama.
9.Mtoto mwanaume wa ndugu mwanaume wa kwa baba tu.
10.Ami (baba mdogo) wa kwa baba na mama (ndugu yake baba).
11.Ami wa kwa baba tu.
12.Mtoto mwanaume wa Ami wa kwa baba na mama.
13.Kijana mwanaume wa Ami wa kwa baba.
14.Mume.
15.Bwana mwenye kumuacha mtumwa huru.
Wenye kurithi wanawake ni hawa:
1.Binti (mtoto mwanamke).
2.Binti wa mtoto mwanaume (mjukuu).
3.Mama.
4.Dada wa kwa baba na mama.
5.Dada wa kwa baba.
6.Dada wa kwa mama.
7.Bibi mzaa baba.
8.Bibi mzaa mama.
9.Mke.
10.Bibi mwenye kumuacha mtumwa huru.
Kuzuiliana
Wanawake na wanaume wakikutana wote pamoja hawawezi kurithi wote bali wachache wakiwepo huwazuilia wengine.
Wanaozuiliwa wanaume
1.Mjukuu huzuiliwa na mtoto mwanaume.
2.Babu wa upande wowote huzuiliwa na baba au babu wa karibu zaidi.
3.Ndugu wa kwa baba na mama huzuiliwa na mtoto mwanaume au mjukuu au baba.
4.Ndugu wa kwa baba huzuiliwa na ndugu wa kwa baba na mama ,Pia huzuiliwa na dada wa kwa baba na mama akiwa pamoja na binti wa mtoto wa kiume (mjukuu) au wote wawili.
Wanaozuiliwa na wanawake
1.Ndugu wa kwa mama huzuiliwa na mtoto au mtoto wa mtoto mwanaume au baba au babu.
2.Bibi huzuiliwa na mama.
Wasiozuiliwa wanaume
1.Mtoto mwanaume.
2.Baba.
3.Mume.
Wasiozuiliwa wanawake
1.Mke.
2.Binti.
3.Mama.
Mafungu yenye kurithiwa (4:11-12)
- Nusu (1/2).
- Robo (1/4).
- Thuluthi (1/3).
- Thuluthi mbili (2/3).
- Sudusi (1/6).
- Thumuni (1/8).
Katika warithi kuna wenye kupata mafungu maalumu katika hayo mafungu sita na kuna wasiokuwa na mafungu maalumu ambao hupata kilichobakia baada ya wenye mafungu kuchukua mafungu yao au hupata mali yote ikiwa hapana wenye mafungu.
Wasio na mafungu katika mirathi huitwa Asaba.
Wenye mafungu maalumu katika urithi ni hawa:
- Baba.
- Babu.
- Binti.
- Binti wa mtoto mwanaume (mjukuu).
- Ndugu wa kwa mama.
- Dada wa kwa baba na mama.
- Dada wa kwa baba.
- Dadad wa kwa mama.
- Mama.
- Bibi.
- Mume.
- Mke.
Asaba
(a) Asaba kwa nafsi yake
Ni wale waume tu ambao uhusiano wao na huyu marehemu haukuingiliwa na mwanamke.Nao ni hawa:
- Mtoto mwanaume.
- Baba.
- Babu.
- Ndugu wa kwa baba na mama.
- Mtoto mwanaume wa ndugu wa kwa baba na mama.
- Mtoto mwanaume wa ndugu wa kwa baba.
- Ami wa kwa baba na mama.
- Ami wa kwa baba.
- Mtoto mwanaume wa Ami wa kwa baba na mama.
- Mtoto mwanaume wa Ami wa kwa baba.
- Bwana na Bibi mwenye kumuacha mtumwa huru.
- Asaba wa mwenye kumuacha huru mtumwa.
(b) Asaba wa pamoja na mtu mwingine
- Binti akiwa pamoja na kijana mwanaume.
- Binti wa mtoto wa kiume (mjukuu) akiwa pamoja na mtoto mwanaume wa mtoto mwanaume (mjukuu wa kiume).
- Dada wa kwa baba na mama akiwa pamoja na ndugu wa kwa baba na mama.
- Dada wa kwa baba akiwa pamoja na ndugu wa kwa baba.
- Dada wa kwa baba na mama au wa kwa baba akiwa pamoja na babu.
(c) Asaba kwa sababu ya mtu mwingine
- Dada wa kwa baba na mama au wa kwa baba tu atakapokuwa pamoja na binti au binti wa mtoto wa kiume au wote wawili.
Musharakah-Kushirikiana fungu
Mfano.Amekufa mtu akaacha mume, mama na ndugu wa kwa mama zaidi ya mmoja na ndugu wa kwa baba na mama.
Ugawaji wa mirathi
Mume atapata nusu (1/2) =3/6
Mama ana sudusi (1/6) =1/6
Ndugu wengine wa kwa mama wanathuluthi (1/3) =2/6
Hapo utaona kuwa mafungu yote sita yamegawanywa yakaisha na ndugu wa kwa baba na mama hawakupata kitu.Hapa itabidi ile thuluthi waliyoipata ndugu wa kwa mama wagawane sawa na ndugu wa kwa baba na mama.Maana na wao wao wanahaki ya ndugu wa kwa mama kama wao na wala hawakoseshwi kwa sababu ya uasaba wao.
Kurithisha kwa kutumia mifano
Swali 1.
Akifa mtu akawa ameacha vijana wanaume wanne.Warithishe kiislamu.
Jibu
Kwa kuwa warithi ni asaba peke yao, mali yote itagawanywa mafungu manne sawa sawa na kila mmoja atachukua fungu lake.
Swali 2.
Amekufa mtu akaacha watoto sita, wanne wanaume na wawili wanawake.Warithishe kiislamu.
Nanma ya kurithisha
Kila mwaume atahesabiwa sawa na wanawake wawili.
Wanaume wanne watahesabiwa sawa na wanawake nane.Hivyo mali itagawanywa katika mafungu kumi yaliyo sawa sawa.
Wanaume watapata mafungu mawili kila mmoja na wanawake watapata fungu moja moja.
Swali 3.
Amekufa mke na kuacha wafuatao:
(i)Mume.
(ii)Mtoto mwanaume.
(iii)Baba.
Rithisha kiislamu.
Namna ya kurithisha
Wenye mafungu maalumu ni hawa:
(i)Mume-Atapata robo (1/4) kwa kuwa kuna mtoto.
(ii)Baba-Atapata sudusi (1/6) kwa kuwa yupo mtoto.
Mtoto wa kiume atapata kitakachobakia.
Ugawaji
Tafuta kigawo kidogo cha shirika cha 4 na 6 (K.D.S) ambacho ni 12.Hivyo kutakuwa na mafungu 12.
(i)Mume =1/4x12=3-mafungu.
(ii)Baba =1/6x12 =2-mafungu.
Mtoto wa kiume=Idadi ya mafungu-mafungu yaliyochukuliwa.
=12-(3+2)
=12-5=7
Kwa hiyo mtoto wa kiume atapata mafungu 7
Swali 4.
Amekufa mume na kuacha wafuatao:
(i)Mke
(ii)Mama
(iii)Mjukuu mmoja wa kike
(iv)Mtoto mwanaume
(v)Watoto watatu wanawake
Ikiwa mali iliyoachwa na marehemu ni shilingi 1,200/=.Rithisha kiislamu.
Namna ya kurithisha
Wenye mafungu maalumu
(i)Mke-Atapata thumuni (1/8) kwa sababu kuna watoto.
(ii)Mama-Atapata sudusi (1/6) kwa kuwepo mtoto.
Mjukuu wa kike hatapata kitu kwa sababu anazuiliwa na mtoto wa marehemu.
Asaba(Mtoto mwanaume+watoto watatu wa kike) watapata kitakachobakia.
Ugawaji
(i)Mke =1/8x1,200=150/=
(ii)Mama =1/6x1,200=200/=
Fedha iliyobakia itagawiwa kwa Asaba
=1,200-(200+150)
=1,200-350
=850
Tutengeneze mafungu.
Mtoto wa kiume=Watoto wawili wa kike
Hivyo kila mtoto wa kike ni fungu.
Idadi ya mafungu =2+3=5
Kila fungu litakuwa na thamani ya shilingi (850÷5=170/=)
Mtoto wa kiume =170x2=340/=.
Watoto wa kike watatu watapata shilingi 170x3=510/=.
Swali 5
Baada ya kuzikwa Abu Dhar ikabainika kuwa marehemu ameacha
watoto wa kiume watano,mabinti sita,wajane watatu pamoja na
wazazi wake wawili.Ameacha pia wadogo zake wanne,wawili
wakiwa wakike na wawili wakiume mmoja kwa baba tu na mmoja
kwa baba na mama.Gawanya mirathi kwa wanaostahiki ikiwa
marehemu ameacha nyumba tatu za kisasa zenye thamani
Tsh.milioni arobaini,duka lenye thamani ya milioni kumi na fedha
taslim laki saba.Pia ameacha wasia kuwa mtoto wake mkubwa wa
kiume apewe nyumba moja.
Dondoo
-Warithi;-
Watoto wa kiume 5
Watoto wa kike 6
Wake 3
Baba
Mama
Dada 2
Kaka 2, kwa baba tu 1,kwa baba na mama 1.
-Mali iliyoachwa;
Nyumba tatu 40,000,000/=
Duka 10,000,000/=
Fedha taslim 700,000/=
JUMLA 50,700,000/=
-Wasia:-mtoto wa kiume apewe nyumba moja
-Mafungu ya kurithi
Dada 2: Hawatarithi chochote kwa sababu kuna watoto wanaowazuilia.
Kaka 2: Hawatarithi chochote kwa sababu kuna watoto wanaowazuilia.
-Wasia:Hautatekelezwa kwa sababu mtoto huyo anafungu maalumu
katika mirathi.
-Wake(wajane) 3:watagawana thumuni(1/8) ya mali aliyoacha
marehemu kwa sababu kuna watoto.
-Watoto:Wa kiume watapata mara mbili ya watoto wa kike:5x2+6=16
-Baba atapata sudusi(1/6) kwa sababu kuna watoto.
-Mama atapata sudusi(1/6) kwa sababu kuna watoto.
-Kwa hiyo;
Baba:1/6x50,700,000/= =8,450,000/=
Mama:1/6x50,700,000/= =8,450,000/=
Wake:1/8x50,700,000/= =6,337,500/= @2,112,500/=
Jumla ya fedha zilizogawanywa 23,237,500/=
-Fedha zilizobaki bado hazijagawanywa:50,700,000-23,237,500=27,462,500/=.
-27,462,500/16 = 1,716,406.30/=.
1,716,406.30x2 = 3,432,812.60/=
-Mgawanyo:
Watoto wa kiume @ =3,432,812.60/=
Watoto wa kike @ =1,716,406.30/=
Wake(wajane) @ =2,112,500.00/=
Baba =8,450,000.00/=
Mama @ =8,450,000.00/=
Maswali
1.Mzee Khalfan alipofariki dunia aliacha binti wawili na kijana mmoja, mkewe na wazazi wake wawili, kama warithi wake pekee.Mali pekee aliyowaachia ni shilingi 170,000/=.Alikwa na deni la shilingi 20,000/= na aliusia shilingi 30,000/= zitolewe sadaka kwa ajili ya kujenga shule ya awali ya kiislamu eneo la Tanesco.Kama ilivyoamrishwa katika Qur’an (4:11-12), gawanya urithi huu kwa kuzingatia wahusika.
2.Amefariki mke na kuacha wafuatao:
(i)Mume
(ii)Dada wawili wa kwa baba na mama.
Ikiwa marehemu ameacha mali yenye thamani ya shilingi 124,000/=.Rithisha Kiislamu.
Umuhimu wa kugawa mirathi Kiislamu
(i)Ni amri na agizo kutoka kwa Allah (s.w) .
(ii)Ni kitambulisho (kigezo) cha imani na ucha Mungu wa mtu/watu.(33:36) na (4:13).
(iii)Kuacha na kukataa kugawa na kugawana mirathi Kiislamu ni mojawapo ya sababu zitakazowapelekea watu kuingia motoni na kupata adhabu zenye kufedhehesha.(4:14).
(iv)Kugawa mirathi Kiislamu ni miongoni mwa sababu zitakazowafanya waumini waingie peponi na wafaulu mbele ya Allah (s.w).(4:13).
Hekima ya sheria ya Mirathi ya Kiislamu
Kutoa haki kwa kila mrithi kwa mujibu wa maagizo ya Allah (s.w).
Kuepusha wasiohusika na mali ya marehemu kugawiwa mali ya marehemu, hivyo warithi stahiki kuepushwa kudhulumiwa haki zao.
Hekima ya watoto wa kike kupata nusu ya watoto wa kiume ni kwamba wanaume wanamajukumu makubwa ikiwa ni pamoja na kuwa mawalii wa dada zao.
Udhaifu wa sheria ya kitwaghuti ya Mirathi
(i) Sheria ya kitwaghuti ya Mirathi inatoa mgawanyo sawa kwa kila mtoto wa marehemu bila ya kujali jinsia.
Udhaifu
Wanaume wana majukumu mengi zaidi katika familia kuliko wanawake.
Kuwagawia sawa wanawake na wanaume ni kumdhulumu mwanaume kwani yeye ndiye mwenye wajibu wa kuhakikisha dada yake anapata mahitaji yote muhimu ikiwa ni pamoja na chakula, mavazi, makazi na elimu.
(ii) Mtoto au watoto wan je ya ndoa hupewa haki ya kurithi sawa sawa na watoto wa ndani ya ndoa.
Udhaifu
Kuondosha umuhimu wa ndoa katika jamii hivyo kuchochea zinaa na madhara yake.
Huchochea migogoro katika familia na kuvunja mahusiano mema ya kibinadamu.
Watoto wa ndani ya ndoa hudhulumiwa haki zao na kupewa watu wasiostahiki.
Hadhi na Haki za mwanamke katika Uislamu
Wanawake na wanaume wana hadhi na haki sawa kutokana na misingi ifuatayo:-
(i) Asili yao ni moja.(4:1), (30:20-21) na (49:13).
(ii) Lengo la kuumbwa kwao ni moja.(51:56), (3:195), (4:124) na (9:72).
(iii) Binadamu wote wanaume na wanawake wamekusudiwa kuwa Makhalifa wa Allah (s.w) hapa ulimwenguni.(2:30-34) na (24:55).
Uislamu haukubaliani na umoja wa sare unaopigiwa zumari na makafiri.
-Kwamba wanawake na wanaume wawe sawa kimavazi, kimahusiano, kimaingiliano, kikazi, kivipaji na maumbile.
-Wanawake na wanaume hawako sawa kimaumbile na kimajukumu.
-Uislamu ni dini ya kweli inayoendana na ukweli wa kimaumbile.
Ni zipi haki za mwanamke katika Uislamu?
1. Haki ya Elimu.
Elimu ni faradhi kwa watu wote.(96:1-5).
2. Haki ya ndoa.
Kukubali kuolewa na mwanaume anayemtaka.
Kuchagua anayemuoa.
3. Haki ya Talaka
Kuomba talaka kama mume hamtendei haki kwa mujibu wa sheria.
Kumtaliki mumewe kama walikubaliana.
4. Haki ya kurithi (4:7)
Watapata kulingana na maelekezo ya Allah (s.w) yaliyobainishwa katika Qur’an.
5. Haki katika sheria
Haki katika sheria za madai na jinai.
Sheria haibagui mwanaume au mwanamke.Mfano mwizi hukatwa kiganja cha mkono.
6. Haki ya kushiriki katika siasa
Jukumu la kusimamisha ukhalifa liko kwa wote
Kuamrisha mema na kukataza mabaya ni jukumu la wanawake pamoja na wanaume.
7. Haki ya uchumi (4:32)
Wanahaki ya kumiliki mali na kutumia kwa mujibu wa sheria.
8. Haki ya kupiga kura
Kufanya Bai’at (kiapo cha utii)kwa kiongozi.
Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za kijahili
Ifuatayo ni Hadhi ya mwanamke katika jamii za kijahili:
Mwanamke ni chombo cha kumstarehesha mwanaume.Mfano wanawake makahaba.
Mwanamke kuonekana kuwa duni na nuksi katika jamii.
Kupata mtoto wa kike ilikuwa ni huzuni na wazazi waliishi kwa huzuni na aibu katika jamii.
Mwanamke kufanywa mali ya mumewe ambaye aliweza kumfanya lolote alitakalo kama anavyofanyiwa mtumwa.
Akili ya mwanamke katika jamii imelinganishwa na ile ya mtoto mdogo, kwa sababu hii mwanamke hakuombwa ushauri wa jambo lolote lile katika familia.
Haki za mwanamke katika jamii za kijahili
Hakuwa na haki ya kurithi.
Alirithiwa kama mali ya marehemu.
Alinyimwa haki za kiuchumi.Hakuwa na haki ya kumiliki mali aliyoichuma mwenyewe.
Watoto wadogo wa kike walizikwa wakiwa hai.(16:58-59).
Mwanaume aliyefiwa na mumewe hakuruhusiwa kuolewa tena.(4:19).
Mwanamke alifanyishwa kazi na kubebeshwa mizigo kama punda.
Alipewa majukumu mengi zaidi kuliko umbile lake.Mfano uzazi, malezi ya watoto na kutafuta mali kwa wakati mmoja.
Hifadhi ya mwanamke katika Uislamu na hekima yake
Mwanamke wa kiislamu anapaswa ajistiri kwa kuzingatia sheria za Allah (s.w) na mafundisho sahihi ya Mtume (s.a.w).(24:31) na (33:59).
Hekima ya hifadhi (stara) kwa wanamke ni:
Kumuepusha kuikurubia zinaa hivyo kuwa mcha Mungu.
Hupandisha hadhi na heshima ya mwanamke katika jamii.
Mwanamke kutobughudhiwa na wanaume katika jamii.
MFUMO WA JAMII YA KIISLAMU.
Misingi na Maadili katika Uislamu
Maadili ni nini?
Maadili ni mwenendo na tabia inayomfikisha binadamu katika hadhi yake ya ukhalifa na kumuwezesha kufikia lengo la kuumbwa kwake.
Vifuatavyo ni vipawa vinavyomtofautisha binadamu na wanyama:
- Elimu
- Akili
- Utambuzi binafsi
- Uhuru
Tofauti kati ya mtazamo wa Uislamu na mtazamo wa Kitwaghuti juu ya maadili
Mtazamo wa Matwaghuti juu ya maadili
(a) Lengo kuu la maisha
- Kuishi maisha yenye furaha.
- Kufikia utimilifu.
- Kila mtu atomize wajibu wake kwa madhumuni tu ya kutimiza wajibu.
(b) Chemchem tunazozitegemea zitutambulishe mema na maovu
- Uzoefu wa binadamu.
- Silika zetu.
- Vipawa vya kufikiri na kuhoji.
(c) Msimamizi wa maadili katika jamii
- Kanuni zinazooana na hoja za akili.
- Serikali kwa kutumia polisi, mahakama na magereza.
(d) Kichocheo kitakachowapelekea watu katika jamii wawe na maadili
- Maumbile ya binadamu.
- Hamu ya kutaka ukamilifu.
- Kutaka hidaya.
- Kuchukia adhabu.
Mtazamo wa Uislamu juu ya Maadili
(a) Lengo kuu la maisha
- Kumuabudu Allah (s.w).(51:56).
- Lengo la vilivyotuzunguka ni kumtumikia binadamu ili afikie lengo la kuumbwa kwake.(2:29).
(b) Chemchem tunazozitegemea zitutambulishe mema na maovu
- Ni Allah (s.w) kupitia vitabu vyake na Mitume wake.(57:25).
- Qur’an na Sunnah
(c) Msimamizi wa maadili katika jamii
- Imani thabiti juu ya Allah (s.w) na siku ya mwisho pamoja na vipengele vingine vya nguzo za Imani.(33:36).
(d) Kichocheo kitakachowapelekea watu katika jamii wawe na maadili
- Kuhofu ghadhabu na adhabu ya Allah (s.w) itakayowafika watu waovu katika maisha ya akhera.(89:25-26).
- Kutarajia msamaha na pepo ya Allah (s.w) katika maisha ya Akhera.(9:111) na (61:10-13).
Misingi ya Maadili ya Kiislamu
(i) Qur’an: Maelekezo ya Allah (s.w).
(ii) Sunnah (Hadith): Mafundisho ya Mtume (s.a.w)
Sheria katika Uislamu
Maana ya sheria
Sheria ni taratibu, kanuni, masharti na amri zenye kutiiwa ambazo huwekwa ili mahusiano ya watu katika jamii inayohusika.
Kazi za sheria katika jamii
- .Kulinda watu na mali zao.
- Kumlinda mwanadamu yeye mwenyewe binafsi dhidi ya madhara ambayo yanaweza kusababishwa na mwenendo wake mbaya.
- Kuhifadhi amani na usalama ili jamii iweze kuishi bila migongano na vurugu.
- Kuhifadhi maadili ya jamii.
- .Kupanga utaratibu juu ya namna ya kuendesha shughuli mbalimbali zenye maingiliano ya kijamii.
Sheria zilizotungwa na wanadamu zinamadhaifu mengi, hivyo haziwezi kuiletea jamii ya mwanadamu maisha ya furaha na amani ya kweli.
Sheria za Allah (s.w) ndizo pekee zenye uwezo wa kuifanya jamii iishi maisha ya furaha na amani ya kweli kwani Allah (s.w) anamfahamu mwanadamu matashi yake, ujanja wake, matatizo yake n.k
Mgawanyo wa makosa na adhabu zake katika sheria ya Kiislamu
1.Makosa ya Hudud
Ni makosa yote yaliyokatazwa na Allah (s.w) na hukumu zake zimetajwa katika Qur’an au Hadith sahihi.Mfano wa makosa ya aina hii ni;
(i) Kuritadi (Riddah)
Ni Muislamu kuukanusha Uislamu kwa maneno yoyote ya Qur’an au kuukataa Uislamu kwa vitendo kama vile kutotoa zakat.
Aliyeritadi hupewa muda wa kutubia na ukipita muda hajatubia hukumu yake ni kuuawa.Qur’an (9:5).
(ii) Wizi
Hukumu yake ni kukatwa mkono.
Mwizi atakatwa mkono wa kulia iwapo yatatimia masharti yafuatayo:
(a) Awe amekusudia kuchukua mali ya wizi pasi na idhini ya mwenye mali.
(b) Awe ameiondosha mali hiyo mahali inapowekwa.
(c) Awe amevunja sefu au kasha au kibweta cha fedha.
(d) Mali iliyoibiwa iwe imefikia angalau thamani ya kima cha chini Nisabu-yaani iwe na thamani sawa na mizani moja.Mizani moja ni sawa na dinar tatu za fedha au robo ya dinar au dirham kumi za fedha.
(e) Mali iliyoibiwa iwe ni halali katika Uislamu.
(iii) Uasi (Baghi)
Ni uasi dhidi ya kiongozi halali wa kiislamu.Kama uasi hauna msingi wowote, waasi watapigwa vita mpaka wajisalimishe.
(iv) Ujambazi (Haraba) (5:33)
- Hukumu kukatwa mikono na miguu kwa mabadilisho.
- Kusulubiwa.
- Kuhamishwa katika nchi (jela).
(v) Uzinzi (24:2)
- Hukumu ni bakora 100 kwa ambao hawajaoa wala kuolewa.
- Hukumu ni kupigwa mawe mpaka kufa kwa wanandoa.
(vi) Kashfa (24:4)
- Msemo, vijembe au maandiko na machapisho yenye lengo la kutoa kejeli dhidi ya kutusi, au kushusha hadhi ya mtu.
- Hukumu ni kuchapwa mijeledi themanini (80).
- Kashfa katika sheria ni kumzulia mtu kuwa kazini au kalawiti au kalawitiwa au kumkashifu mtu muadilifu, mwenye akili timamu na uwezo wa kimwili wa kutenda kosa alilozuliwa.
(vii) Kunywa ulevi (5:90)
- Hukumu kuchapwa bakora arobaini (40).
2 .Makosa ya Qisasi
Ni yale yanayompa mdhulumiwa haki ya kulipa kisasi kwa Yule aliyedhulumu.
Kisasi ni kumfanyia vile vile kama alivyokufanyia katika kudhulumu.(2:178)
Aina zake;
(a) Makosa ya kuua . (5:45)
(b) Makosa ya kujeruhi. (4:92)
3. Makosa ya Taazir
Ni makosa yote ambayo Qur’an na Sunnah hazijaweka adhabu maalumu.
Hukumu yake hutegemea maamuzi ya jaji au hakimu kwa kulinganisha kosa, mazingira ya kosa na adhabu.
Tofauti ya chimbuko la sheria za Kiislamu na zile za Kitwaghuti
(a) Chimbuko la sheria za Kitwaghuti
- Zimetungwa na mwanadamu kutokana na vipawa vya kufikiri na kuhoji.
- Mila na desturi zilizozoeleka.
Nguvu za dola hugawanywa katika maeneo makuu matatu ambayo ni;
- Chombo cha kutunga sheria (Bunge)
- Chombo cha utendaji (Serikali)
- Chombo cha kutafsiri sheria na utoaji haki (mahakama).
(b) Chimbuko la sheria ya Kiislamu
- Kitabu cha Allah (s.w) (Qur’an) na Sunnah.
Kwa waislamu Qur’an ndio katiba yetu na ndiyo msingi wa sheria zote.Uamuzi wowote unaokiuka Qur’an ni batili na hauwezi kukubalika.
- Ijtihad (Qiyas na Ijmaa).
Misingi ya sheria katika Uislamu
(i) Ufalme wote ni wa Allah (s.w). (59:23) na (5:45)
(ii) Utii kwa Mitume wa Allah (s.w). (4:64) na (4:80)
Haki za makundi ya watu mbalimbali katika Dola ya Kiislamu
(a) Haki za mshitakiwa wakati wa upelelezi
- Haki ya kutokamatwa na kupekuliwa ovyo.
(b) Haki za mshitakiwa wakati wa kuhojiwa
- Wanaohoji wawe wawili.Mkuu wa malalamiko na Mwendesha mashtaka.
- Mtuhumiwa katika makosa ya Hudud na Qisas ana haki ya kutoapa.
- Katika uchunguzi wa makosa ya Hudud anayohaki ya kukataa kuhojiwa, na anayohaki ya kukaa kimya.
- Mtuhumiwa asiteswe au kufanyiwa ukatili.
- Mahojiano yawe ya kibinadamu, ili mtuhumiwa akiri kosa lake kwa hiari bila kulazimishwa.
(c) Haki za mshitakiwa wakati wa kusikilizwa kesi
- Afunguliwe mashtaka haraka na ahukumiwe.
- Ushahidi katika makosa ya Hudud ni wa kisheria na si wa rai.
- Anayo haki ya kulipwa fidia ikiwa atahukumiwa kimakosa.
- Ashitakiwe katika mahakama yenye mahakimu wenye ujuzi na waadilifu.
- Mtu yeyote pamoja na kiongozi wa nchi anaweza kujibu shitaka mahakamani.
- Mshitaki na mshitakiwa wote wana haki ya kumteua mtu wa kuwawakilisha mahakamani (wakili).
Kila raia ana haki ya kuhukumiwa kwa uadilifu. (5:8) na (4:135).
Uchumi katika Uislamu
Tofauti kati ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na ule wa kikafiri
Maana ya uchumi
Ni utaratibu wa maisha unaohusiana na uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa mali na huduma.
Uchumi wa Kiislamu ni utaratibu wa maisha unaohusiana na uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa mali na huduma kwa kuzingatia mipaka na miiko iliyowekwa na Qur’an na Sunnah.
Zifuatazo ni tofauti kati ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na ule wa kikafiri.
Mfumo wa uchumi wa Kiislamu
Mfumo wa uchumi wa Kikafiri
1.Dhana ya mafanikio
Mafanikio hupimwa kwa kuzingatia upatikanaji wa radhi za Allah (s.w) na kufeli hupimwa kwa kiasi gani mtu amekosa radhi za Allah (s.w)
1.Dhana ya mafanikio
Mafanikio hupatikana kwa kulimbikiza mali nyingi bila ya kujali halali na haramu katika mchakato mzima wa kuchuma.
2.Dhana ya umilikaji mali
Mmiliki wa mali na rasilimali zote ni Allah (s.w) na binadamu amemilikishwa tu kama amana na ataulizwa jinsi alivyochuma.
2.Dhana ya umilikaji mali
Mmiliki wa mali na rasilimali zote katika ardhi ni binadamu
3.Utumiaji wa mali
Binadamu ataulizwa jinsi alivyotumia mali.
Itatumiwa kwakuzingatia mipaka iliyowekwa na Allah (s.w)
3.Utumiaji wa mali
Binadamu ana uhuru wa kutumia mali apendavyo
4.Dhana ya bidhaa
Ni vile tu vilivyo halali kutumiwa kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah
4.Dhana ya bidhaa
Ni chochote kinachohitajiwa na kutumiwa na watu bila ya kuzingatia uhalali na uharamu
Njia za Halali za uchumi na za Haramu
Njia za uchumi za halali ni njia zote ambazo zimehalalishwa na sheria ya Uislamu yaani hazipingani na mafundisho ya Qur’an na Sunnah.
Njia za uchumi zilizoharamishwa ni njia zote ambazo zimeharamishwa na Qur’an au Sunnah.Zifuatazo ni njia za uchumi haramu:
- Wizi wa aina yoyote
- Ulevi wa aina yoyote
- Kamari.(5:90) na (2:219).
- Hongo na rushwa
- Kutoa na kupokea riba
- Kipato chochote kinachotokana na utengenezeji wa sanamu na picha za watu na wanyama.
- Kipato chochote kutokana na umalaya, ngoma na muziki wa aina yoyote.
- Kipato chochote kutokana na utabiri, ramli na upigaji bao.(5:90).
Uharamu wa riba na madhara yake
Riba ni kiasi cha ziada anachotoa mtu wakati wa kurejesha kile alichokopa bila ya kuzingatia faida au hasara.
Kwanini uislamu umeharamisha riba?
- Riba ni dhulma (unyonyaji).Matajiri wanapaswa kuwapatia wanyonge na wenye dhiki mahitaji yao muhimu ya maisha, sio kuwapa mzigo wa kulipa.
- Riba inahamisha mali kutoka kwa maskini au wanyonge na kuipeleka kwa tajiri ambayo huzidi kuondoa usawa katika mgawanyo wa mali.
- Riba hufanya kundi la watu katika jamii liishi kivivu bila ya kufanya shughuli yoyote ya uzalishaji, likitegemea kuishi kwa riba kutokana na mali zao walizozikusanya katika mabenki, bima na vyombo vingine vya riba.
Madhara ya riba katika jamii
(i) Riba inachafua nafsi ya tajiri na uchumi wake
- Kutotoa mali yake bure kuwasaidia wanyonge na wenye dhiki.
- Kutochunga mipaka ya kuchuma mali.
(ii) Riba inamkandamiza mnyonge mwenye dhiki
- Kujipatia chakula katika mapipa ya taka, kukaa stesheni na masokoni.
- Hujiona hawa maana.
(iii) Riba inaharibu uchumi wa jamii na maendeleo yake
(iv) Riba ni mali ya dhulma inayonyakuliwa na matajiri kutoka kwa wanyonge, hivyo inaukandamiza na kuudidimiza uchumi wa taifa na kimataifa.
(v) Kuibuka kwa kundi la watu wavivu na wazembe wenye kutegemea riba tu kutoka katika mabenki, hivyo rasilimali watu hupotea.
(vi) Kuimarika na kuwepo kwa tofauti kubwa ya hali ya kimaisha baina ya wenye navyo na wasiokuwa navyo.
Biashara Haramu
Biashara inaweza kuwa haramu kwa namna mbili:
- Kutofuata misingi ya Halali iliyowekwa na Allah (s.w) na Mtume wake.
- Biashara iliyoharamishwa moja kwa moja hata kama misingi ya halali itafuatwa.
Biashara zilizoharamishwa moja kwa moja ni hizi zifuatazo:
(i) Muzabanah-Kunufaika kibiashara kutokana na matatizo ya watu.
(ii) Mu’awamah-Uuzaji wa matunda na mazao mengine ya shambani kabla hayajakomaa kiasi cha kufaa kuliwa.
(iii) Hablul-Habalah-Kuuza kilichotumboni katika wanyama kabla hakijazaliwa.
(iv) Uuzaji wa bidhaa kabla hazijamfikia mnunuzi.
(v) Ununuzi wa bidhaa njiani kabla ya wauzaji hawajafika sokoni.
(vi) Kununua bidhaa iliyonunuliwa na mtu mwingine kwa kulipa bei kubwa zaidi au kwa sababu zinginezo.
(vii) Kuuza maji au majani asili ambayo mtu hakuyagharimikia chochote.
(viii) Uuzaji wa samaki aliyoko majini, uuzaji wa ndege anayeruka angani, uuzaji wa maziwa ambayo hayajakamuliwa, uuzaji wa manyoya yangali mwilini mwa mnyama.
(ix) Uuzaji na ununuzi wa damu, uuzaji wa uhuru wa mtu, uuzaji wa nywele za binadamu na uuzaji wa maziwa ya binadamu.
(x) Uuzaji na ununuzi wa mbwa, nguruwe, pombe, damu, mizoga na vyote vilivyo haramishwa.Pia uuzaji wa masanamu na picha za watu na wanyama.
(xi) Ulanguzi (kuhodhi bidhaa).Ununuzi wa bidhaa kwa wingi na kwa bei ya juu ili kuihodhi na kuifanya iwe adimu ili baadaye uuze kwa bei ya juu unayotaka.
(xii) Kupunja vipimo.
(xiii) Kuficha ila (dosari) ya bidhaa inayouzwa.
Namna ya kuendesha taasisi za fedha kwa kufuata sheria za Kiislamu
Benki ni Taasisi za fedha ambazo ni muhimu sana katika uchumi kwa kutoa huduma zifuatazo:
- Kuhifadhi akiba za watu na mali zenye thamani kubwa kama vile dhahabu na madini mengine yenye thamani kubwa.
- Kukopesha watu mitaji ya kufanyia shughuli mbalimbali za uchumi.
- Kurahisisha malipo kwa njia ya hundi (cheque) kwa kuwalipa wafanyakazi kupitia benki zao.
- Kutoa huduma ya kupokea malipo kupitia matawi ya benki husika kote nchini au ulumwenguni.
Benki za Kiislamu
Hutoa huduma bila ya kutoza au kutoa riba.Hufanya kazi kwa namna hizi:
(a) Kukopesha bila riba kwa muda watakaokubaliana na wakopaji kwa kuweka au kutoweka rehani.
(b) Kushirikiana katika mtaji na kugawana gharama za uendeshaji, faida na hasara kwa namna ifuatayo:-
(i) Mudharabah
- Ni makubaliano kati ya wawili au zaidi ya kuingia katika ushirika ambapo mmoja anatoa mtaji na mwingine hushiriki kikamilifu katika uendeshaji wa mradi huo wa uchumi.
- Kugawa faida kwa mujibu wa makubaliano.
- Hasara inakuwa kwa mwenye kutoa mtaji.
(ii) Musharikah
- Ni hali ya watu wawili kushiriki katika kuchangia mtaji na uendeshaji lakini si lazima watoe hisa zilizo sawa kwa makubaliano ya kugawana faida na hasara kwa uwiano wa hisa walizotoa.
(iii) Ijara -Uara wa Iktina
- Mtu au benki inatumia fedha zake katika kukodi vitu kama vile magari,majumba na ardhi ambavyo vikifanyiwa kazi huzalisha mali na kutoa faida.
(iv) Murabah
- Ni utaratibu wa kununua bidhaa kwa wingi kwa ajili ya kuwauzia kwa faida wafanya biashara walioagiza kuwa bidhaa hizo zinunuliwe kwa ajili yao.
(v) Muqaradhah
- Ni kitendo cha kununua “shares” au” bonds” katika kampuni za uzalishaji kwa mapatano ya kugawana faida na hasara kulingana na kiasi cha “share”au “bond”.
Siasa na uendeshaji wa Dola.
Maana ya siasa na Dola kwa mtazamo wa kikafiri
Maana ya siasa
- Ni sayansi ya maongozi ya jamii.
Maana ya siasa kwa mtazamo wa Uislamu ni dhana ya mpangilio wa uendeshaji mambo kijamii ambayo hutokana na itikadi ya mtu, kikundi cha watu au ufunuo toka kwa Muumba.
Dhana kuu za siasa ni ; utawala(mamlaka), itikadi, matashi na maamuzi.
Mifumo mikuu ya siasa (2:257)
1. Mfumo wa siasa wa Kiislamu
Ni utaratibu ni utaratibu na muongozo wa masuala ya jamii ambao misingi yake ni kitabu cha Allah (s.w) na Sunnah za Mitume wake tangu Adamu mpaka Muhammad (s.a.w).(23:23) na (11:50).
2. Mfumo wa siasa wa Kitwaghuti
Ni utaratibu wa maongozi ya kijamii uliobuniwa na watu.Mifano:
- Ujima wa mwanzo
- Utumwa
- Umwinyi
- Ubepari
- Ujamaa na ukomonisti
- Demokrasia
Dola ni eneo la ardhi lenye mkusanyiko wa watu waliochini wa utawala mmoja wenye uwezo wa kujitosheleza kwa mahitaji muhimu na kulinda mipaka ya eneo lake.
Eneo hili la ardhi huitwa nchi na wakazi wake huitwa wananchi au raia.
Msonge wa uongozi katika Uislamu
(a) Msonge wa uongozi katika Dola ya Kiislamu wakati wa Mtume (s.a.w)
- Allah (s.w)
- Mtume Muhammad (s.a.w)
- Shura (sekretarieti ya Mtume)
- Viongozi wa mikoa na viongozi wengine katika ngazi na Nyanja mbalimbali.
- Ummah wa Kiislamu (wenye mchanganyiko wa Mayahudi, wakristo na washirikina).
(b) Msonge wa uongozi katika jamii yoyote ya Kiislamu
- Allah (s.w)-Qur’an
- Mtume (s.a.w)-Sunnah (Hadith)
- Majlis shura (Bunge)
- Viongozi wa jamii wa ngazi zote (Taifa hadi familia)
- Ummah wa Dola ya Kiislamu.(Waislamu na wasiokuwa waislamu)
Kazi za bunge la Kiislamu
Bunge ni chombo cha kushauriana juu ya masuala mbalimbali ya Dola ya Kiislamu
Zifuatazo ni kazi za bunge la Kiislamu:
Huitafsiri sheria na kuiweka sheria itokanayo na Qur’an na Sunnah katika mazingira ya utekelezaji.
- Pale ambapo Qur’an na Sunnah zinamaelezo yenye tafsiri zaidi ya moja, bunge huchagua moja ya tafsiri hizo na kuidhihirisha kutumika katika jamii kama rejea iliyokubalika.
- Pale ambapo hukumu za Qur’an na Sunnah haziko wazi, bunge hupitisha fat-wa ya kufuatwa na jamii.
- Kutoa fat-wa kuhusiana na hali za dharura zinazojitokeza kisiasa, kiuchumi n.k.
Msonge wa uongozi wa serikali za Kibunge (Parliamentary form of government)
- Bunge
- Waziri mkuu/Raisi
- Baraza la mawaziri
- Wakuu wa majimbo (Mikoa)
- Watendaji mbalimbali
Msonge wa uongozi wa serikali chini ya Raisi (Presidential form of government)
- .Raisi.
- Waziri mkuu.
- Wabunge.
- Baraza la mawaziri.
- Wakuu wa majimbo (Mikoa).
- Watendaji mbalimbali.
Sifa za kiongozi katika Uislamu
- Awe mjuzi wa Qur’an na Sunnah na mjuzi wa kitengo anachotakiwa akiongoze.
- Awe muislamu mcha Mungu
Mcha Mungu ni Yule anayeishi kwa kuchunga mipaka ya Allah (s.w) na kujitahidi kwa jitihada zake zote kufuata maamrisho yote ya Allah (s.w) na kuacha makatazo yake yote.
3 Awe na tabia njema.Huruma, subira, hekima na uadilifu.
4 .Awe na sifa (afya) nzuri.(2:247).
Haki mbalimbali za raia katika Dola ya Kiislamu
(a)Haki zinazomstahiki kila binadamu
- Haki za kuishi.
- Haki ya usalama wa maisha.
- Haki ya kuheshimu usafi wa wanawake (Utoharifu).
- Haki ya kupata mahitaji ya lazima ya maisha.
- Haki ya uhuru.
- Haki ya uadilifu katika hukumu.
- Haki ya usawa.
- Haki ya uhuru wa mahusiano.
- Haki ya heshima.
- Haki ya usalama na uhuru wa mtu binafsi.
(b) Haki za Raia katika Dola ya Kiislamu
- Haki ya kuendesha maisha ya Binafsi.
- Haki ya uhuru wa kutoa maoni na kuamrisha mema na kukataza mabaya.
- Haki ya uhuru wa kufuata dini yoyote.
- Haki ya kuabudu.
- Haki ya kuwashitaki viongozi wa juu wa Dola.
- Haki ya kupinga udhalimu.
(c) Haki za wasiokuwa waislamu katika Dola ya Kiislamu (Dhimi)
- Haki ya ulinzi wa maisha na mali.
- Haki katika sheria za jinai.
- Haki katika sheria za madai.
- Haki ya heshima.
- Haki katika sheria ya mtu binafsi.
- Haki ya kuabudu na kupewa heshima mahali pakuabudu.
- Haki ya kusamehewa kushiriki katika vita vya jihadi.
Dhimi hawana haki ya kuongoza katika Dola ya Kiislamu kwa sababu hawakubaliani na lengo kuu la Dola ya Kiislamu.
QUR’AN
Ithibati ya Qur’an
Madai ya makafiri wa leo dhidi ya Qur’an na udhaifu wa madai hayo
(i) Qur’an ni mashairi aliyotunga Muhammad(s.a.w)
Udhaifu
- Historia inakanusha dai hili.Mtaalamu wa mashairi Labiid bin Rabia alikiri kuwa Qur’an si mashairi na alisilimu baada ya kusoma aya chache zilizo kuwa zimebandikwa Al-Kaaba.
- Kutojua kusoma na kuandika kwa Muhammad(s.a.w)
- Qur’an ni ujumbe wenye maana kamili ulioandikwa katika fasihi ya hali ya juu kwa kuzingatia sarufi na miiko yote ya lugha hai.Mashairi yana beti ,vina,mizani na yanaimbika kiasi kwamba wakati mwingine hata maana na sarufi huwekwa pembeni alimradi shairi liimbike,Qur’an haiku hivyo
(ii) Qur’an ni zao la njozi za Mtume(s.a.w) zilizo vurugika
Udhaifu
- Katika historia nzima ya mwanadamu hapajatokea mawazo ya kinjozi hata yawe yamebuniwa kwa uhodari kiasi ganiS yakaunda kitabu mithili ya Qur’an.
- Wanadamu wenye mawazo yaliyo tulia na weledi kushindwa kauandika kitabu mithili ya Qur’an
(iii) Qur’an ni zao la mwenye kudhania kupata ufunuo
Udhaifu
- Endapo chimbuko la Qur’an ni hisia za ndani za nafsi ya Muhammad(s.a.w),basi Qur’an itakuwa inatokana na elimu na mazingira yake.Lakini Qur’an imetoa taarifa nyingi sana ambazo itakavyokuwa vyovyote haziwezi kuwa zimetoka katika nafsi ya Muhammad(s.a.w).
(iv) Qur’an ni zao la mwenye kifafa na aliyepagawa na shetani
Udhaifu
- Je,kifafa ugonjwa ubaya kama tunavyoufahamu,umewahi kumtokea mtu katika historia ya mwanadamu nabado akawa mtu mwenye kutoa sharia za na umati wa watu wengi zaidi ya robo dunia?
- Je,historia kufuatwa ya mwanadamu imewahi kumshuhudia mgonjwa wa kifafa au mwenye kupagawa na shetani kuwa na hadhi na uwezo mkubwa kuliko mtu yeyote ulimwenguni kama ilivyokuwa kwa Mtume(s.a.w)?
- Kama mgonjwa wa kifafa ndiye aliyeandika Qur’an,inakuwaje waandishi hodari wenye akili timamu na wanafalsafa wakubwa washindwe kuandika kitabu mithili ya Qur’an?
(v) Qur’an ni aya za shetani
Udhaifu
- Ujumbe wa Qur’an umeteremshwa ili kumuokoa mwanadamu kutokana na hadaa zote za shetani(2:208)
- Allah(s.w) amebainisha kuwa laiti ingelikuwa Qur’an hii ingetoka kwa asiye kuwa Allah(s.w) basi ndani yake kungekuwa na Ikhtilafu nyingi(mgongano wa aya).(4:82)
- Qur’an yenyewe imekataa dai hilo (81:25)
- IIwapo kiumbe dhaifu kama shetani ameweza kuandika kitabu chenye ujumbe mzito kama Qur’an na kutoa changamoto kwa binadamu wa zama zote iweje wataalamu waliopo washindwe walau kujibu changamoto hizo?
- Qur’an aya zake nyingi zinadai”Shetani ni adui yenu mfanyeni adui”kama shetani ndiye”mwandishi” kwanini ajiseme vibaya hivyo?.
(vi) Muhammad(s.a.w)alitunga qur’an ili kuleta umoja na ukombozi wa waarabu
Udhaifu
- Lau hilo lingekuwa la kweli basi hapana shaka kuwa Qur’an ingetia msisitizo mkubwa sana katika mada ya umoja na ukombozi wa waarabu.Hakuna hata aya moja inayozungumzia jambo hili.
- Msingi wa ummah(taifa) unaofundishwa na Qur’an umejengwa juu ya itikadi ya haki na Qur’an inapinga hisia zote za utaifa kwa kufuata misingi ya rangi au kabila.
- Lau umoja wa waarabu ungekuwa ndio jambo lililomsukuma Muhammad(s.a.w) kutunga Qur’an hapana shaka angekubali kuwa mfalme wa waarabu ili atumie fursa hiyo kujenga umoja wa taifa la waarabu.
- Zipo aya katika Qur’an zinazolikanusha dai hilo.(3;42) na (2:47)
(vii) Ni utunzi wa Muhammad(s.a.w) ili kurekebisha tabia ya waarabu
Udhaifu
- Kujenga mwenendo mzuri wa tabia za watu ni jambo jema ambalo laweza kutekelezwa pasi na kutumia udanganyifu na uovu mwingine.Ni kipi kilicho mfanya Muhammad(s.a.w) atumie uwongo na udanganyifu ili awafundishe watu kuwa wakweli na waaminifu?
- Qur’an imeitaja dhambi ya kuzua uwongo kuwa ni miongoni mwa madhambi makubwa.(6:93).
(vii) Muhammad(s.a.w) ili ajinufaishe kiuchumi.
Udhaifu
Mtume(s.a.w) alikuwa na hali nzuri ya kiuchumi kabla ya utume kuliko baada ya kupata utume.
Mtume(s.a.w) kila alipopata zawadi aliigawa yote kwa mafakiri bila yeye mwenyewe kuchukua chochote.Safari moja alipewa na chifu wa Fidak zawadi zilizobebwa na ngamia wane,lakini alizigawa zote.
Wakati anafariki Mtume(s.a.w) hakuwa hata na senti moja mfukoni.
(viii)Muhammad(s.a.w)alitunga Qur’an ili kuwania Madaraka na ukubwa.
Udhaifu
- Muhammad(s.a.w)alijulikana sana ulimwengu mzima kama kiongozi aliye fanikiwa sana katika historia ya binadamu.Mtu mwenye sifa kama hizo angeweza kuchukua uongozi na madaraka bila hata kudai kwanza utume.Kwa hakika kufanya hivyo kungekuwa rahisi zaidi kwake kama alikuwa anataka madaraka,kuliko kudai utume kwanza.
- Qur’an imetamka wazi kuwa hakuna mtu yeyote ikiwa ni pamoja na Muhammad awezaye kuleta mfano wake.Angejitapa kuwa ndiye mtunzi wa kitabu hiki kinachivishinda vitabu vyote.
- Tabia yake haikuonesha dalili zozote za mtu anayepigania madaraka au utukufu.
(ix) Mtume Muhammad (s.a.w) aliandika Qur’an kwa msaada wa Mayahudi na Wakristo.(10:103), (44:14) na (25:4).
-Mhunzi wa kiyahudi ambaye ni Jabir
-Mkristo wa Sham ambaye ni Salman
Udhaifu
- Kutofautiana lugha kati ya Jabir na Muhammad(s.a.w) .Lugha ya Jabir ni kiyahudi na lugha ya Muhammad ni kiarabu(16:103)
- Kutojua kusoma na kuandika kwa Muhammad(s.a.w)
- Kutoeleza wazi kwa Muhammad(s.a.w) kuwa amefundishwa na Jabir kwani Muhammad ni mkweli na mwaminifu.
- Dai hili linapingana na historia, kwani katika historia yake hakuna mahali popote tunapofahamishwa kuwa alikaa kitako kwa mtu yeyote kujifunza chochote.
- Theluthi mbili ya Qur’an ilishuka Makka kabla Mtume (s.a.w) hajahamia mMadina ambapo alikutana na Salman.
- Fasihi ya lugha liyotumika katika Qur’an ni ya hali ya juu mno kiasi ambacho wanafasihi mashuhuri wa kiarabu walijaribu kwa miaka mingi kuigiza Qur’an bila ya mafanikio yoyote, itakuwaje Mfursi awe ndiye aliyeiandika?.
Hoja zinazothibitisha kuwa Qur’an ni neno la Allah (s.w)
(a) Qur’an ni kitabu cha Allah(s.w) kutokana na Qur’an yenyewe.
- Kutojua kusoma na kuandika kwa Mtume(s.a.w) .(7:158)na (29:48)
- Qur’an yenyewe kujieleza kuaw ni ktabu cha Allah(s.w) katika aya chungu nzima.(4:166),(32:2-3),(25:1) na (45:2)
- Hali aliyokuwa nayo Mtume(s.a.w) katika kupokea wahay.Alikuwa akiharakia wahay akijua kuwa atasahau.(75:16-18) na (87:6-7)
- Qur’an kushuka kidogo kidogo kwa kipindi cha miaka 23.(17:106),(25:32) na (76:23).
- Kukosolewa Mtume(s.a.w) ndani ya Qur’an.(33:1-3),(66:1) na (80:1-12)
- Kutokea kweli matukio yaliyotabiriwa katika Qur’an.(93:4-5).(94:5-6),(30:2-6),(48:1) na (111:1-5).
- Kuhifadhiwa Qur’an katika mas-hafu.Sura moja kuwa na aya zilizoshuka katika nyakati tofauti.
- Mpangilio wa Qur’an
- Maudhui ya Qur’an na mvuto wa ujumbe wake
- Wanadamu kushindwa kuandika kitabu mithili ya Qur’an.(17:18),(11:13),(2:23) na (10:38).
(b) Qur’an ni kitabu cha Allah (s.w) kutokana na Historia (Hadith)
- Tukio la pango la Hira-Mtume (s.a.w) kushtuka kwa kutembelewa na Malaika Jibril (a.s) na kukhofu kwa kiasi kikubwa sana.
- Mtume (s.a.w) alikuwa anabadilika haiba yake na kutokwa na jasho wakati wa kupokea wahay.
Sura zilizoteuliwa (Tyn, Nashrah, Dhuha, A’alaa).
Mwanafunzi aweze kufanya yafuatayo:
- Kusoma na kuhifadhi sura zilizoteuliwa.
- Kutafsiri na kuchambua mafunzo yatokanayo na sura zilizoteuliwa.
1.SURATUT-TIN (95:1-8)
Tafsiri
Kwa jina la Allah,Mwingi wa Rehma,Mwenye kurehemu
1.Naapa kwa tini na zaituni
2.Na kwa mlima Sinai
3.Na kwa mji huu(wa makkah) wenye amani
4.Bila shaka tumemuumba mwanadamu kwa umbo lililo bora kabisa.
5.Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini
6.Ila wale wenye kuamini na kutenda mema,watakuwa na ujira usiokwisha(unaoendelea maisha).
7.Basi ni lipi likupalo kukadhibisha malipo baada(ya kuona hayo)?
8.Je!Allah si hakimu muadilifu kuliko mahakimu wote?
Mafunzo kwa muhtasari
Allah(s.w) ameapia mazingira waliomotokea mitume wakembalimbali,ili kwa kuzingatia ujumbe wa Mitume hao,uwe ni chachu kwa wasomaji kutafakari juu ya ujumbe unaofuatia.
Ubora wa binadamu hupatikana kutokana na imani sahihi iliyoambatana na vitendo vizuri
Mwanadamu akiamua kufuata maisha ya kumkufuru na kumuasi Mola wake,huwa muharibifu katika jamii kuliko wanyama waharibifu
Malipo ya kumuamini Allah(s.w) na kufuata muongozo wake hapa duniani ni kuishi kwa furaha na amani(maisha ya nuru)
Malipo ya kumkufuru na kumuasi Allah(s.w) na kufuata miongozo iliyo dhidi na uongozi wake hapa duniani ni kuishi maisha ya Khofu na dhulma(maisha ya giza)
Lazima iwepo siku ya mwisho ili waumini waliotenda vitendo vizuri na makafiri waliofisidi katika ardhi walipwer kwa uadilifu jaza ya vitendo vyao.
2.NASHRAH (94:1-8)
Tafsiri
Kwajina la Allah Mwingi wa Rehma Mwenye kurehemu.
1.Je,hatukukupanulia kifua chako.
2.Na tukakuondolea mzigo wako(mzito).
3Uliovunja mgongo wako?
4.Na tukakutukuza utajo wako?
5.Basi kwa uhakika baada ya dhiki (huja faraja)
6.Hakika baada ya dhiki huja faraja.
7.Basi ukisha maliza (kulingnia)shughulika kwa ibada nyingine.
8.Najipendekeze kwa mola wako.
Mafunzo kwa muhtasari
Hatuna budi kushukuru neema mbalimbali alizoturuzuku Allah(sw)kwa kujizatiti kuifundisha na kuisimamisha dini yake katika jamii.
Yeyote yule atakayedhamiria kuujua uislamu kwa usahihi na kuingiza katika utendeji katika undeshaji maisha yake ya kila siku,uoni wake maisha na wa masuala ya jamii utakuwa ni wajuu kuliko ule wa watu wengine.
Muumini wa kweli anawajibu wa kuondoa maovu na dhuluma katika jamii na kusimamisha wema na uadilifu.
Kwamtazamo wa uislamu ,mwenye kuheshimika mbele ya ya waumini si yule mwenye hadhi kubwa katika jamii kicheo au kimali;bali yule aliye mstari wa mbele katika kuufuata uislamu na kuusimamisha katika jamii.
Wakati wowote waislamu watakapojitahidi kuufahamu uislamu vilivyo, kuutekeleza na kuusimamisha katika jamii,na wakasubiri juu ya magumu yanayowafika ,Allah(sw)atawafanyia wepesi kwa kila hatua wanayoipiga kusonga mbele na hatimaye atawawezesha kusimamisha uislamu katika jamii kama alivyomuwezesha mtume(s.a.w)na maswahaba zake.
Hakuna wakati wa kupoteza kw muislamu.kama muislamu hana la maana la kufanya amdhukuru mwenyezi mungu kwa kuleta tasbihi mbalimbali
3.DHUHA (93:1-11)
Tafsri
Kwajina la Allah Mwingi wa Rehma Mwenye kurehemu
1.Naapa kwa mchana.
2.Nakwa usiku unapotanda.
3.Hakukuacha mola wako wala hakukukasirikia (ewe nabii Muhammad).
4.Nabila shaka (kila)wakati ujao (utakuwa)bora zaidi kuliko uliotnglia .
5.Na mola wako atakupa mpaka uridhike.
6.Je,hakukukuta yatima akakupa makazi (mazuri ya kukaa)?
7.Na akakukuta hujui kuongoza njia, akakuongoza? 9Basi usimuone yatime.
10Wala usimkalipie aulizaye.
8.Na akukuta fakiri akakutajirisha?
11.Na neema ya mola wako usimulie(kwa kushukuru na kufanya amali njema)
Mafunzo kwa Muhtasari
Mwenyezi mungu huapia viumbe vyake, ili hivyo viumbe kwa namna vinavyojulikana view ni ushahidi au dalili ya wazi ili kuyakinisha jambo linaloelezwa baada ya kiapo hicho
Hakuna kipindi chochote cha harakati za kuhuisha na kusimamisha uislamu ambacho mtume (s.aw)hakuwa na msaada wa Allah (sw).
Pamoja na hali duni ya waliyonayo waislamu hivi sasa, wakifanya jitihada za kuujua uislamu, kuutekeleza na kuufundisha kama alivyofanya mtume(s.aw)na maswahaba zake katika kipindi kigumu cha makka, .
Muislamu anatakiwa awe na tabia kuwaangalia walio chini yake kila hali na mali na usiwangalie waliojuu yake ili aweze kukinai juu ya neema alizoneemeshwa na mola wake na kuwahurumia wale walio chini yake.
Mwenyezi mungu pekee ndiye mthibiti wa mafaniko au shida .Huibadili hali moja hadi nyingine wakati wowote apendavyo.
Hatuna budi kumshukuru Allah (sw)kwa kila neema tuipatayo na njia bora ya kushukuru neema ni kuitumia neema hiyo kwa kuujibu wa maagizo ya mwenyezi mungu na kuzidisha dhikiri na ibada za aiada kama vile kukithirisha swala za suna , visimamovya usiku ,funga za sunna, kutoa sadaqa , n.k. Neema kubwa tuliyopewa ni kuwa waislamu.
4.SURATUL-A’ALAA (87:1-19)
Tafsiri
Kwajina la Allah Mwingi wa Rehma Mwenye kurehemu.
1.Litukuze jina mola wako aliyemtukufu
2.Aliyeumba (kila kitu)na akakitengeza.
3.Na akakikadilia (kila kimoja jambo lake)na akakiongoza.
4Na aliyeotesha ndisha (malisho)
5Kisha akaifanya mikavu yenye kupiga weusi.
6.Tunakusomesha wala hutasahau.
7.Ila akipenda mwenyezi mungu ;yeye anajua yaliyodhiri na yaliyofichikana.
8.Nasi tutakusahilishia (kuitangaza)dini iliyo nyepesi (uislamu)
9.Basi waidhisha ikiwa utafaa waadhi.
10.Bila shaka atakumbuka mwenye kumuogopa Allah(sw)
11.Na mwingi wa mateso atajitenga mbali nayo hayo(mawaidha)
12.Ambaye atauingia moto mkubwa
13.Kisha humo hatakufa wala hatakuwa hai
14.Hakika amekwisha faulu aliyejitakasa na mabaya
15.Akakumbuka jina la Mola wake na akaswali
16.Lakini nyinyi mnapenda zaidi maisha ya dunia
17.Haliyakuwa ya Akhera ni bora(zaidi kabisa) na yenye kudumu
18.Hakika haya(mnayoambiwa humu katika Qur’an) yamo katika vitabu vilivyo tangulia.
19.Vitabu vya Ibrahi na Mussa
Mafunzo kwa muhtasari
Allah(s.w) pekee ndiye anayestahiki kutukuzwa na kusifiwa kwa sababu ndiye aliyeumba kila kitu na kukitengeneza katika sura maridhawa kwa lengo maalumu.
Qur’an imehifadhiwa na Allah(s.w) na ameijalia kuwa nyepesi kwa yule anayetaka kuongoka na akatia juhudi ya kuisoma na kuifuata.
Uislamu ni dini nyepesi kuijua na kuifuata
Kila muislamu anawajibu kuujua Uislamu vilivyo na kuutekeleza
Kila muislamu anawajibika kuufundisha na kuufikisha ujumbe wa Uislamu kwa wale ambao haujawafikia na kuwaonya na kuwakumbusha wale uliowafikia wakapuuzia au kusahau.
Wale watakao pokea ujumbe wa Uislamu wakajitakasa na maovu na wakajizatiti kumtukuza Mola wao katika kila kipengele cha maisha yao watakuwa ni wenye kufuzu katika maisha ya dunia na akhera.
Wale watakao puuza mafundisho ya Uislamu wakatakabari na kuendelea kufanya maovu watastahiki adhabu ya Allah(s.w) iumizayo katika maisha ya Akhera,japo hapa duniani wanaweza kuonjeshwa starehe ndogo.
Maisha ya Akhera ndio bora kwani ni yenye starehe ya kweli yenye kudumu milele.
Uislamu ni dini pekee ya Allah(s.w) kwa ajili ya walimwengu wote wa nyakati zote.
7.SUNNAH NA HADITH
Hadith zilizoteuliwa.
Mafunzo yatokanayo na Hadith zilizoteuliwa.
1.Uislamu wapiga vita rushwa
Kutoka kwa Thaubaan (r.a) kasema: Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w):
“Mwenyezi Mungu amemlaani mtoa rushwa, mpokea rushwa na mtu wa kati baina ya mtoaji na mpokeaji rushwa (wakala)”.(Ahmad)
Mafunzo ya Hadith
Jambo lolote analolifanya mja likafisadi kupatikana uadilifu ni rushwa.
Hakuna maendeleo ya Ummah na jamii pale penye wala rushwa kwani rushwa inaondosha ubinadamu na kuleta tabia za kinga za kutokuwa na haya na kutojali.
2.Kila mmoja wetu afanye kazi (asiwe omba omba)
Kutoka kwa Abdillahi bin Umar (r.a) amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w):
“Mtu ataendelea (na tendo lake) la kuomba omba mpaka itafika siku ya kiyama (afufuliwe) na uso wake usiwe na kipande cha nyama”.
Mafunzo ya Hadith
Kufanya kazi yenye manufaa na halali.
Kila mwenye uwezo wa kufanya kazi afanye kazi na awahimize wengine kufanya kazi.
Adhabu inawangojea wavivu, waombaji na wazururaji.
Uislamu unawahimiza waislamu kufanya kazi zilizo halali, na ku acha kufanya kazi wakati mtu anao uwezo wa kufanya hivyo ni kinyume na Uislamu.
3.Kiongozi katika Uislamu
Kutoka kwa mtoto wa Sayyidna Umar (r.a) hakika Mtume (s.a.w) amesema:
“Bila shaka, nyote ni viongozi na mnadhamana kwa mnaowaongoza na mtaulizwa juu ya mnaowaongoza.Hivyo amiri (kiongozi mkuu) ni dhamana, nae ataulizwa kuhusu raia zake, mwanaume (baba) anadhamana kuwahusu watu wa nyumbani kwake, naye ataulizwa juu yao,na mwanamke (mama) ana dhamana kuhusu nyumba ya mumewe na wanawe, naye ataulizwa kuwahusu, na mtumishi ni mdhaminiwa
mali ya bwana wa mali ya bwana wake naye anawajibika juu yake, Hakika nyote ni dhamana na nyote mtawajibika juu ya mnao waongoza”.(Bukharin a Muslim)
Mafunzo ya Hadith
Umuhimu wa kutekeleza haki na wajibu, na kugawana majukumu baina ya wanajamii.
Kuwakomboa wanawake na wafanyakazi wote ili wazalishe kirahisi.
Kuwa na mpango mzuri wa utawala unaojali usawa, haki na maendeleo ya Taifa.
4.Kumtii kiongozi
Kutoka kwa Ibn Umar (r.a) kasema: Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w):
“Ni wajibu kwa muislamu kusikiliza na kufuata maamrisho ya kiongozi wake kwa anayoyapenda au anayoyachukia maadamu hakuamrishwa mambo ya maasi.Iwapo ataamrishwa kufanya maasi asisikile wala asifuate.”(Bukhari).
Mafunzo ya Hadith
Viongozi wanaochaguliwa na umma wanakuwa chini ya matakwa yao (watu) wanahaki ya kuwakosoa na kuwazindua.
Ni wajibu wa ummah wote kuwatii viongozi wao wanaohukumu kwa uadilifu.
8.HISTORIA YA UISLAMU BAADA YA KUTAWAFU MTUME (S.A.W) HADI HIVI LEO
Ukuaji na Uendeshaji wa Dola ya Kiislamu wakati wa Makhalifa wane waongofu
Makhalifa wanne waongofu na taratibu zilizotumika kuwapata
Mtume (s.a.w) ametawafu siku ya jumatatu mwezi kumi na mbili Rabiul Awwal mwaka wa 632 au mwaka wa 11 Hijiria, akiwa na miaka 63.
Pamoja na kuwa Mtume (s.a.w) aliumwa tangu miezi michache lakini ugonjwa uliokuwa sababu ya kifo chake ulichukua siku kumi na tatu hivi, akazidiwa na kutawafu siku hiyo.
Wafuatao ni Makhalifa walioongoza Dola ya Kiislamu baada ya kutawafu Mtume (s.a.w)
1.Abubakar Siddiq (r.a) 11-13 A.H
2.Umar bin Khattab (r.a) 13-24 A.H
3.Uthaman bin Affan (r.a) 24-36 A.H
4.Ali bin Abu Talib (r.a) 36-41 A.H
Zifuatazo ni taratibu zilizotumika kuwapata Makhalifa waongofu:
1.Kuchaguliwa Abubakar (r.a) kuwa Khalifa
Mtume (s.a.w) hakuusia nani awe khalifa.
Abubakar (r.a) alipendekezwa na Umar (r.a) katika ukumbi wa Thaqifah bani Saidah, walipokuwa wamekutana Ansar kwa ajili ya suala la kutafuta kiongozi baada ya Mtume (s.a.w) kutawafu.
Wote waliokuwa ukumbini walikubali pendekezo la Umar (r.a) na kumpa Abubakar (r.a) mkono wa ahadi ya utii (Bai’at).
Suala hili lilipopelekwa msikitini waislamu wote waliridhia na waislamu 33,000 walimpa Abubakar (r.a) mkono wa ahadi ya utii.
Abubakar (r.a) alistahiki kuchukua nafasi ya ukhalifa kwa sifa zifuatazo:
(i)Alikuwa na sifa zote za msingi za kiongozi wa kiislamu.
Ucha Mungu
Ujuzi wa Qur’an na Sunnah
Siha nzuri
Tabia njema
(ii)Alikuwa mtu mzima wa kwanza kusilimu na alikuwa karibu sana na Mtume (s.a.w) kuliko swahaba mwingine yeyote.(9:40).
(iii)Mtume (s.a.w) alimteua kuongoza swala kwa niaba yake alipokuwa mgonjwa kitandani karibu na kutawafu kwake.
Siku moja Umar (r.a) aliswalish kwa kuwa Abubakar alichelewa, Mtume (s.a.w) aliwaamrisha maswahaba wairudie swala ile na aswalishe Abubakar (r.a).
(iv)Alikuwa mtu mashuhuri anayekubalika, mtaratibu, mwenye Istiqama na Ikhlas, mpevu wa uoni na mwenye maamuzi na alikuwa mfuasi wa nyayo za Mtume (s.a.w).
(v)Alikuwa na umri mkubwa zaidi kuliko wale waliokuwa pale Thaqifah bani Saidah.
Sababu zilizopelekea Riddah
Habari za kutawafu Mtume (s.a.w) zilipelekea makabila mengi ya kiarabu yaliyokuwa chini ya Dola ya Kiislamu kuasi.
Dola iligawanyika katika makundi ya watu yafuatayo:
(i)Wale waliobakia na Uislamu bila kutetereka hasa watu wa Makka, Madina na Taifu.
(ii)Wanafiki
(iii)Wale waliobakia na Uislamu lakini walikataa kupeleka zakat Madina kwenye baitul mal.Walidai kuwa watawasadia wasiojiweza katika maeneo yao.
(iv)Wapo waliobaki Waislamu lakini walikataa nguzo ya zakat
(v)Wako walioritadi na kurudi kwenye dini zao za awali.
(vi)Waliojitangazia utume na wakapata wafuasi.
Zifuatazo ni sababu zilizopelekea uasi:
(i)Udhaifu wa Imani.Wale waliokataa kupeleka zakat Madina na waliokataa kutoa kabisa.(49:14).
(ii)Husuda na uroho wa madaraka.Waliodai utume.
(iii)Kulinda maslahi na kuondokana na kulipa zakat.Walioritadi.
(iv)Kulinda hadhi zao na nafasi zao katika koo zao na mila zao.Walioritadi.
(v)Kutolipa jizya na kurudisha utukufu wao wa kikabila.Ambao hawajasilimu na walifanya mkataba wa amani na Dola ya Kiislamu.
Kukomeshwa kwa uasi
Waislamu walipambana na makundi yote yaliyotangaza uasi dhidi ya Dola ya Kiislamu na makundi yote yalisalimu amri na kuendelea kuwa na utii chini ya Dola ya Kiislamu.
Kazi ya kuzima uasi iliongozwa na Hudhafa, Arfaja na Ikrima.
Mitume wa uongo waliozuka ni hawa;
Aswad Aus
Tulaiha
Sajah bint Alharith
Musailamah Al-kadh-dhab (Mzandiki)
2.Kuchaguliwa kwa Khalifa wa pili Umar bin Khattab (r.a)
Abubakar (r.a) alipokaribia kutawafu aliitisha shura yake na kumpendekeza Umar (r.a) achukue uongozi wa Dola ya Kiislamu baada yake.Alimpendekeza kwa kuzingatia ucha Mungu wake na msimamo wake juu ya Uislamu.
Baadhi ya wajumbe wa shura ya Abubakar (r.a) ni hawa:
Umar bin Khattab (r.a)
Uthmani bin Affan (r.a)
Zaid bin Thabit (r.a)
Abdur Rahmani bin Auf (r.a)
Muadh bin Jabal (r.a)
Ubay bin Ka’ab (r.a)
Wajumbe wawili walihofia juu ya ukali wa Umar (r.a).Abubakar (r.a) aliwatoa wasiwasi na kuonesha kuwa kutokana na Ucha Mungu wake na kazi yenyewe ya ukhalifa itamfanya awe mpole.
Baada ya shura yake kumuunga mkono, Abubakar (r.a) aliandika usia na ukasomwa msikitini kasha akapanda kwenye mimbari na kuhutubia ummat wa Waislamu kama ifuatavyo:
“Enyi ndugu zangu, sikumchagua kuwa khalifa ukoo wangu, nimemteua aliyebora miongoni mwenu, mnakubaliana na uteuzi wangu?”
Waislamu wote waliitikia kwa kukubali.
3.Kuchaguliwa kwa Uthman (r.a) kuwa Khalifa wa tatu
Kipindi hiki kulikuwa na watu sita waliolingana sifa nao ni hawa:
(i)’Uthman bin Affan (r.a)
(ii)Ali bin Abu Talib (r.a)
(iii)Saad bin Waqqas (r.a)
(iv)Talha (r.a)
(v)Zubair (r.a)
(vi)Abdur-Rahman bin Auf (r.a)
‘Umar alichagua jopo la watu hawa sita na akawausia kuwa katika muda wa siku tatu baada ya kifo chake wawe wameshamchagua khalifa miongoni mwao.
Katika siku ya tatu baada ya kufariki ‘Umar, ‘Abdur-Rahman bin Auf, alijitoa kwenye jopo la kuchaguliwa ili aweze kusimamia uchaguzi wa khalifa kutokana na wale wanne waliokuwepo-(Talha alikuwa safarini).
Katika mchakato wa uchaguzi, Ali (r.a) alimpendekeza ‘Uthman na ‘Uthman alimpendekeza Ali (r.a), ambapo Zubair na Saad walimpendekeza ‘Uthman.Hivyo ‘Uthman (r.a) alipata kura 3 na Ali (r.a) kura 1.
Siku ya nne, ‘Abdur-Rahman alimtangaza ‘Uthman kuwa ndiye khalifa naye akawa wa kwanza kumpa bai’at, ndipo waislamu wengine waliokuwa msikitini walifuatia kumpa bai’at.
4.Kuchaguliwa kwa Ali (r.a) kuwa Khalifa wa nne
Baada ya miaka sita ya kwanza ya uongozi wa ‘Uthman (r.a), alizusha fitna ‘Abdullah bin Sabaa, Myahudi aliyesilimu kwa uwongo mkazi wa Yemen.
Katika fitna hizo lilitokea kundi la kupinga uongozi wa ‘Uthman na hatimaye likamuua ‘Uthman.
Hili kundi la wauaji lilimchagua Ali (r.a) kuwa khalifa.
Baadhi ya Waislamu, kwa walivyomfahamu ‘Ali (r.a) bila kuhusisha tukio la kuuliwa ‘Uthman walimkubali na kumpa bai’at.
Wengi wa maswahaba walikuwa tayari kumpa bai’at lakini kwa sharti la kuwashughulikia wauaji kwanza.
‘Ali alikataa kutekeleza sharti hili na Waislamu wakagawanyika katika makundi manne yafuatayo:
(i)Wafuasi wa ‘Uthman-ambao walitaka Dola iwaadhibu wauaji.Wengi wenye msimamo huu walikuwa watu wa Syria na Basra.
(ii)Marafiki wa ‘Ali-hawa ndio lile kundi lililomuua ‘Uthman , watu wa mji wa kufa na Wamisri.
(iii)Mashibah-Hawa walikuwa kwenye jihadi wakati ‘Uthman anauawa hawakuuunga mkono makundi mawili hapo juu.
(iv)Ahli-Sunnah wal-Jamaah-lilikuwa na maswahaba wengi na lilienea Dola yote ya Kiislamu.Kwa msimamo wao waliona kuwa ‘Uthman na ‘Ali wote ni maswahaba waongofu na waliona wote walifaa kuwa makhalifa na kama kuna aliyefanya makosa aliyafanya kutokana na jitihada yake katika mchakato wa utendaji.
Uongozi wote wa Ali (r.a) ulikuwa wa migogoro na wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na hatimaye naye aliuliwa.
Ufuatao ni utaratibu wa kupata viongozi wa Kiislamu:
Kuteua au kupendekeza kiongozi na kupitishwa na waumini (waislamu).Makhalifa hawa walipatikana kwa njia hii; Abubakar na Umar.
Kuteuliwa watu wengi wenye sifa sawa na kupigiwa kura.Khalifa Uthman alipatikana kwa njia hii.
Sababu zilizopelekea kutanuka kwa Dola ya Kiislamu
(i)Mafundisho ya Uislamu kufahamika kwa wepesi na kutekelezeka.
(ii)Waislamu walifanya kazi kubwa ya kulingania Uislamu na kuufundisha kwa ari na hamasa kubwa kwa kutarajia malipo kutoka kwa Allah (s.w).
(iii)Dola ya Kiislamu kupambana na maadui wa Dola hiyo waliodhamiria kuidondosha katika vita na hatimaye kuwashinda maadui.Maeneo yaliyokuwa chini ya maadui yakawa chini ya himaya ya Dola ya Kiislamu na wananchi wake wakaanza kulipa jizya.Huduma zilizotolewa ziliwavutia wananchi wakawa wafuasi halisi wa Uislamu.
(iv)Maadili na wema wa wananchi katika Dola ya Kiislamu yalipelekea watu waupende Uislamu na waishi kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu jambo ambalo lilipelekea kutanuka kwa Uislamu na Dola yake.Haki kutendeka na misingi imara iliyowekwa na Allah (s.w) na kufundishwa na Mtume (s.w) ya kuimarisha maadili.Uislamu ulimvutia kila mwenye kuuona ukitekelezwa.
(v)Umoja na mshikamano wa waislamu uliojengwa juu ya Kalima tukufu ya “Lailaha ila llah”.(61:3-4).
Mfumo wa uongozi, uchumi, ulinzi na mahusiano ya kimataifa
(a)Mfumo wa uongozi
Wajibu wa Khalifa
Khalifa katika serikali ya kiislamu ndiye mtendaji mkuu wa serikali.
Kazi kuu ya khalifa ilikuwa kusimamia utekelezaji wa madhumuni ya kuwepo Dola ya Kiislamu ambayo ni:
(i)Kuhuisha, kuendeleza na kudumisha maadili mema ambayo hupelekea watu katika jamii kuishi kwa furaha na amani.
(ii)Kuzuia na kukomesha maovu ambayo huleta vurugu, mashaka na huzuni katika jamii.
Kazi (wajibu) wa khalifa katika Dola ya Kiislamu
Kujenga maisha ya binadamu juu ya misingi ya ucha-Mungu na matendo mema.
Kutumia uchumi wa Taifa kwa kukuza na kuendeleza maadili mema kwa raia wake.
Kuamrisha mema na kukataza maovu
Kulinda mipaka ya nchi (Dola) kwa gharama yoyote ile,kwa vita au diplomasia.
Kwa kushirikiana na shura yake,atateua viongozi wa serikali katika majimbo.(Magavana,polisi n.k)
Yeye ndiye mkuu wa majeshi na mwenye wajibu wa kusaini mikataba.
Yeye ndiye mwanasheria mkuu wa Dola.
Katika kuendesha shughuli za kila siku za serikali,khalifa alisaidiwa na shura.Khalifa akishirikiana na shura walifanya mambo yafuatayo:
Kupanga mishahara ya wanajeshi.
Kuanzisha idara mbalimbali
Kuwapa vibali wageni kufanya biashara katika Dola ya Kiislamu na kiwango cha kodi wanachotakiwa kulipa
Pamoja na shura makhalifa walikuwa na vyombo vingine walivyovitumia katika kuendesha Dola kama:
Kamati ya utendaji iliyokuwa ikikutana kila siku katika msikiti wa Mtume (s.a.w).
Shura ya watu wote msikitini ilitumika kama chombo cha kusaidia utendaji.
Tume ya kufuatilia malalamiko ya raia dhidi ya viongozi.Mfano alisikiliza malalamiko ya wananchi kila ijumaa.Tume iliundwa ilikuwa chini ya Muhammad ibn Muslamah Ansar.
Mkutano wa watendaji wote wa serikali waliokuwa wanakutana baada ya Hija.
Serikali ilitoa mishahara mikubwa ili kuzuia rushwa na mambo yanayolingana na rushwa.
Wakati wa ukhalifa wa Umar kiongozi alipoteuliwa aliorodhesha mali zake na ilipoonekana anaongezeko la mali lisiloeleweka aliulizwa na mali yake kutaifishwa.
Kama ilivyokuwa wakati wa Mtume (s.a.w) Dola iligawanywa kwenye majimbo na wilaya.Kila jimbo na wilaya lilikuwa na viongozi walioteuliwa na khalifa wafuatao:
(i)Walii-Gavana
(ii)Amil-Mkusanyaji wa mapato ya serikali
(iii)Kadhi-Jaji (mwanasheria)
(b)Uchumi wa serikali ya kiislamu wakati wa makhalifa
Kulikuwa na msimamizi wa mapato ya serikali (Shaikh Ul-kharaj).
Vifuatavyo ni vyanzo vya mapato serikali vya serikali ya Kiislamu:
Zaka na Sadaka.
Ushur: Kodi inayotolewa na waislamu wenye ardhi katika kiwango cha 10% ya mavuno ambayo maji yake ya kumwagilia ni ya asili, na kwa wale ambao mashamba yao hayakuwa ya maji ya asili kwa kumwagilia walilipa 5%.
Jizya : Ni kodi waliyolipa wasiokuwa waislamu wanaume tu wenye uwezo wa kuwa askari.Kwa ajili ya ulinzi wa mali na wao wenyewe.
Al Kharaj: Ni kodi inayolipwa na wasio waislamu, walio na mashamba katika Dola ya kiislamu.
Al-fay: Ni mapato yaliyotokana na mashamba ya serikali kama vile shamba la Fadak.
Al-Ghanima (ngawira): Ni mapato yaliyokuwa yakitokana na mali iliyotekwa katika vita.
Zaraib: Kodi za muda zilizotozwa kwa manufaa ya Dola.
Wakfu, karlaz au kodi kwenye ardhi ya serikali na kodi za madini.
Mali inayoingia nchini au inayopitishwa nchini.
Pia ulianzishwa mfuko wa pato la serikali (Baitul mal).
Maendeleo kutokana na uongozi wa makhalifa ni haya:
(i)Ulijengwa mfereji(canals) wa kutoa maji kutoka mto Euphrates hadi Basra kulikuwa na ukame wa maji.Wakati wa khalifa Umar.
(ii)Ujenzi wa misikiti.
(iii)Ujenzi wa kambi za wanajeshi.
(iv)Ujenzi wa barabara.
(v)Ujenzi wa majengo ya ofisi za serikali na majengo ya ofisi za fedha.
(vii)Ujenzi wa visima.
(viii)Ujenzi wa madaraja.
(c)Ulinzi na usalama wakati wa makhalifa
Ulinzi uliimarishwa kwa kiwango kikubwa.Licha ya kuwa kila muislamu ni askari wa Dola ya Kiislamu,yalianzishwa majeshi maalumu.Mfano ;
(i)Jeshi la Polisi: Lilianzishwa wakati wa khalifa Umar (r.a).Sahib Al-Ahdath (mkuu wa polisi).Maafisa kadhaa waliteuliwa.
(ii)Jeshi la magereza: Magereza ilianzishwa wakati wa khalifa Umar (r.a)
Idara hizi zilianzishwa ili kupunguza makosa na kusimamia haki katika jamii.
(iii)Jeshi la maji.Lilianza katika ukhalifa wa Uthman (r.a).
Kulikuwa na askari wa farasi na askari wa miguu.
Idara ya usalama ilikuzwa zaidi ikilinganishwa na wakati wa Mtume (s.a.w).
(d)Mahusiano ya kimataifa
Dola ya kiislamu ilikuwa na uhusiano mzuri na nchi za nje.
Zifuatazo ni kanuni zilizobainishwa na Qur’an juu ya uhusiano na nchi za nje na namna Makhalifa walivyozitumia:
Kukamilisha mikataba (Ahadi) na muda wake ukiisha wahusika waarifiwe. (9:4), (8:58), (17:34), (16:91) na (16:94).
Misingi ya haki idumishwe kwa wakati wote nje na ndani ya nchi. (5:8).
Utaratibu wa amani daima udumishwe. (8:61).
Kuzuia ufisadi na kujitukuza. (28:83).
Kuwa na uhusiano wa kirafiki na nchi zisizo na ushari. (60:8).
Kuwatendea wema walio wema. (55:60).
Kulipa ubaya kwa walioanzisha ubaya. (42:40-42).
Sababu zilizopelekea kuanguka kwa Dola ya Kiislamu na mafunzo yatokanayo
(a)Sababu zilizopelekea kuporomoka Dola ya kiislamu iliyoasisiwa na Mtume(s.a.w).
Wanafiki walioongozwa na Abdallah bin sabaa,walitunga shutuma za uongo dhidi ya Khalifa ‘Uthman na serikali yake.Hivyo likaibuka kundi la kupinga uongozi.
Abdallah bin sabaa alianzisha imani mpya kuwa kila mtume ana mrithi na mrithi wa Mtume(s.a.w) ni ndugu yake Ali.Makhalifa waliotangulia hawakuwa wa halali.
Kundi la khawarij liloongozwa na Abdallah bin sabaa liliandaa jeshi na kumvamia kahalifa Uthman na kumuua.Kuuawa kwa Uthman (r.a).
Kundi la wauaji lilimchagua Ali kuwa khalifa.Waislamu walitaka wauaji washughulikiwe na waadhibiwe.Ali alikataa kutekeleza jambo hili na ummah wa kiislamu ukagawanyika makundi manne.
Kuzuka vita vya waislamu kwa waislamu.
-Vita vya ngamia.Jeshi la Bibi ‘Aisha(r.a) na jeshi la Khalifa ‘Ali.
-Vita kati ya khalifa Ali na gavana Mu’awiya
Kuuawa Khalifa ‘Ali bin Abi Twalib na kundi la khawarij 17,Ramadhan 40A.H.Mtoto wake Hassan alichaguliwa kuchukua nafasi ya baba yake.
Muawiya aliandaa jeshi dhidi ya Hassan na Hassan akasalimu amri.Alipokaribia kufa Muawiya alimrithisha mtoto wake Yazid kuwa khalifa na huo ndio ukawa mwanzo wa tawala za kifalme(Banu Umayyah).
(b)Mafunzo tunayoyapata kutokana na mambo yaliyopelekea kuanguka kwa Dola ya kiislamu.
Wanafiki ni maadui wakubwa sana wa Uislamu na waislamu hivyo tuchukue tahadhari juu yao.
Fitna ni jambo baya sana hivyo tunapaswa tuzizime kwa gharama zozote zile ili kuepusha madhara katika jamii.
Waislamu hawapaswi kugawanyika kwa namna yoyote ile kwani wakigawanyika nguvu yao itapotea na uislamu utadondoka.
Kupigana vita waislamu kwa waislamu ni jambo baya na ni sababu ya kuharibikiwa katika mambo yetu yaliyostawi.
Tunapaswa kushikamana na Qur’an na Sunnah kwani mafundisho yaliyo nje ya vitabu hivi yatatufanya tuangamie na tuhiliki duniani na Akhera.
Kiongozi wa kiislamu hatokani na ukoo au kuwa na ukaribu na kiongozi aliye tangulia,bali kiongozi wa kiislamu hupatikana kutokana na sifa za kiongozi kama zilivyobainishwa katika Qur’an na Sunnah.
Ni haramu na ni makosa makubwa sana kumpindua kiongozi halali wa kiislamu ambaye bado anafungamana na mwongozo wa Qur’an na Sunnah na kumuua.
Uanzishwaji wa makundi ya harakati ya kuhuisha Uislamu ulimwenguni.
Makundi mbalimbali maarufu ya harakati za kuhuisha Uislamu
(1)Kikundi cha Badee-U-Zaman Said Nursi wa Uturuki
Hiki ni kikundi cha harakati za kuhuisha Uislamu kilichoasisiwa na Badee-U-Zaman aliyezaliwa Hizan, Uturuki, mwaka 1873 A.D.
Lengo kuu la kikundi hiki ilikuwa ni kuutawalisha Uislamu katika ardhi ya Uturuki na kurejesha heshima ya Qur’an kuongoza maisha ya jamii.
Mbinu
(i)Kuanzisha chama cha Ittihadil-Muhammad kikiwa na malengo ya kuleta umoja, uhuru na kusimamisha Uislamu.
(ii)Kuandika na kusambaza makala ambazo zilielezea malengo na program za chama chao na kuwaonya waislamu kuwa endapo watafuata mwongozo mwingine wa maisha usiokuwa Qur’an na Sunnah, basi wajue kuwa wanakaribia maangamizi.
(iii)Kuanzisha chuo kikuu cha Kiislamu.Lengo kutoa elimu ya mazingira na mwongozo kwa lengo la kusimamisha Ukhalifa.
(iv)Kuwalingania watu wote uislamu ikiwa ni pamoja na wabunge.
(v)Kulingania Uislamu kwa kutegemea malipo kutoka kwa Allah (s.w)
Mafunzo
(i)Ujasiri na kukamatana na lengo.Vitimbi na mateso havikuwayumbisha wala kuwatoa kwenye lengo.
(ii)Nafasi ya Elimu.Kuanzisha taasisi za elimu ili watu waelimike na kulijua lengo.
(iii)Mwenendo mzuri.Badee-U-Zaman na wafuasi wake walikuwa ni watu wa maadili mazuri ya kuigwa katika jamii.
(iv)Subira na kukamatana na lengo.Pamoja na mateso na wakati mwingine vishawishi vya kupewa maslahi, hawakutoka katika lengo la kuifundisha na kuisimamisha Qur’an.
(ii)Kikundi cha Ikhwan Muslimiina cha Misri
Muasisi wa kundi hili ni Shahiid Hassan al-Bannah (1906-1949).Alianza harakati hizi za kuhuisha Uislamu akiwa na umri wa miaka 22 baada ya kupata stashahada ya elimu.
Lengo la Harakati ni kusimamisha Uislamu Misri ambapo sheria za Allah (s.w) zitatawala katika kila kipengele cha maisha ya waislamu.
Hali ya waislamu ilivyokuwa kipindi hicho ni kama ifuatavyo:
Palikuwa na wimbi la kuingia Umagharibi ambalo liliathiri sana utamaduni wa Uislamu Misri.
Utenganishaji wa Dini na serikali uliingizwa Misri.
Vishawishi vya zinaa kama vile sinema, kumbi za dansi na madanguro viliota mizizi Misri.
Uislamu ulibakia kuwa suala la mtu binafsi.
Mbinu
(i)Kuanzisha mafunzo maalumu ya kuwalea wanaharakati.
(ii)Kuwaelimisha watu kwa njia ya Mihadhara.
(iii)Kuwaelimisha watu kwa njia ya Mawaidha misikitini.
(iv)Kuwaelimisha watu kwa njia ya maaandishi.
(v)Kuwafikishia ujumbe viongozi wa serikali juu ya hatari ya kuufuata umagharibi na faida za wao kuamua kuufuata Uislamu.
Mwaka 1948 serikali ilipiga marufuku chama cha Ikhwan na wanaharakati wakawekwa ndani na kufilisiwa mali zao.
Hassan al-Bannah aliuawa kwa kupigwa risasi 12/02/1949.
(3)Ikhwan Muslimiina Sudan
Harakati zilianza kwenye miaka ya 1950 katika chuo kikuu cha Khartoum kasha zilienea kwenye vyuo vingine hadi shule za sekondari.
Mwaka 1963, Dr. Hassan Turabi alirudi kutoka masomoni Ufaransa na kukabidhiwa khatamu za uongozi wa harakati za Ikhwan Muslimiina Sudan.
Mbinu
(i)Kuingia ndani ya serikali na kuibana ielekee kwenye kusimamisha Dola ya Kiislamu.1980 wanaharakati wengi walikuwa wana nyadhifa nyeti serikalini na hatimaye Rais Jafar Nimeir kutangaza serikali ya Kiislamu.
(ii)Kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu na ulazima wa kusimamisha sheria ya Kiislamu.
(iii)Kuanzisha chama cha siasa –National Islamic Front (NIF).
(iv)Kuimarisha Uchumi.Kuanzisha makampuni makubwa na Benki kubwa za Kiislamu ndani na nje ya Sudan.
(4)Jamiatil-Islamy cha Pakistani
Mwanzilishi wake ni Sayyid Abdul-A’ala Maududi (1903-1979) aliyezaliwa 25/09/1903 Aurangabag, Pakistani.Kikundi hiki kilianzishwa mwaka 1941.
Mbinu
(i)Kuchapisha magazeti na majarida yanayohusu Uislamu.
(ii)Kuchapisha na kusambaza vitabu vya Kiislamu.Mfano, Katika kuufahamu Uislamu, Tatizo la Kadian (1953) na Uislamu na Kudhibiti Uzazi (1962).
(iii)Kutumia redio kuuneza Uislamu.
(iv)Kujenga na kuendesha taasisi za elimu katika viwano mbalimbali.
(v)Kutoa huduma za jamii kama vile huduma za Afya, kuwasaidia wenye njaa na waliofikwa na maafa.
Mafunzo yatokanayo na jitihada za makundi ya kuhuisha Uislamu
Yafuatayo ni mafunzo yatokanayo na vikundi vya Harakati za kuhuisha Uislamu Misri, Sudan na Pakistan:
Harakati za Kiislamu ili zifikie kilele kinachotarajiwa hazinabudi kufanywa na vijana wasomi wenye nguvu na maarifa ya kutosha.Tusimtarajie mtu kuwa mwanaharakati baada ya kustafu kazi na akawa hana linguine la kufanya.
Misukosuko katika harakati za kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii ni kiashirio cha mafanikio.Bila misukosuko Uislamu hauwezi kusimama katika jamii.(33:22), (2:214) na (3:142).
Mbinu za harakati zinatofautiana kutokana na mazingira.
Kazi kubwa ya msingi katika harakati za kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii ni kutoa elimu ya mazingira sambamba na elimu ya mwongozo.
Hatunabudi kuwa waangalifu katika kuanzisha vikundi vya harakati.Wanaharakati wapatikane kupitia darasa duara na mafunzo maalumu kupitia program maalumu kasha wawekwe kwenye daraja (grade) kulingana na uwajibikaji wao pamoja na kujitoa kwao muhanga na ujasiri wao dhidi ya kupambana na magumu.
Kuingia kwa Uislamu Tanzania na Afrika Mashariki
Namna Uislamu ulivyoingia Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla
Kwa karne nyingi yamekuwepo mahusiano ya kibiashara ya pwani ya Afrika Mashariki na Asia.
Wafanya biashara toka Saudi Arabia, India na nchi za Ghuba walizitumia pepo za misimu (Monsoon Winds) kutembelea Afrika Mashariki kwa shughuli za kibiashara tangia karne ya 8A.D.Kufikia karne ya 9A.D wahamiaji toka Saud Arabia walifanya makazi ya mwanzo hko Benadir katika Pwani ya Somalia.lifundisha Uislamu kwa wakazi wa Pwani ya Afrika Mashariki.
Alama za kale za kuonesha kuwepo kwa Uislamu katika Pwani ya Afrika Mashariki ni magofu ya :
Msikiti wa Kaole-Bagamoyo.
Msikiti wa Kizimbazi-Dimbani Mkoa wa Kusini Unguja-Ulijengwa 500 A.H (1107 A.D).
Magofu ya msikiti wa Kilwa Kisiwani.
Ibn Batuta alipotembelea Afrika Mashariki kwa mara ya pili, 1332 A.D, Miji ya Pwani hasa kilwa ilikaliwa zaidi na Waislamu.
Mchanganyiko wa wageni wa kiarabu na wenyeji wa miji mbalimbali ulipelekea kuzuka lugha ya Kiswahili, yenye mchanganyiko wa kiarabu na kibantu.
Miji ya Unguja, Tanga, Dar es Salaan, Mombasa, Lamu, Malindi na Mikindani iliibuka kuwa vituo muhimu vya kueneza Uislamu katika miji mbalimbali ya bara ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Zaire, Msumbiji, Malawi na Burundi.
Tokea Unguja na miji ya Pwani misafara ya biashara ya waarabu na waswahili iliingia miji ya bara, na kila walipofanya makao walijenga misikiti.
Kutokana na fursa walizopata Waislamu wenyeji kufanya biashara na Waislamu wageni, miji mingi ya Afrika ya Mashariki ilikaliwa zaidi na Waislamu waliomiliki biashara za maduka na magari ya usafirishaji wa abiria na mizigo.
Kwa bahati mbaya Uislamu haukufundishwa kwa lengo la kutawala maisha ya jamii.
Nguvu ya Uislamu ilivyokuwa kabla, wakati na baada ya ukoloni nchini Tanzania na Afrika Mashariki
Uislamu ulikuwa na nguvu kubwa kabla ya ukoloni kwani sehemu mballimbali zilitawaliwa na Waislamu zilikuwa zinautekeleza Uislamu na zilikuwa tayari kukabiliana na maadui wa Uislamu hata kivita pale inapobidi.Mfano, Rejea vita vya maji maji, Bushiri wa Pangani na wajerumani na chifu Isike wa Unyanyembe Tabora.
Uislamu ulikuwa na nguvu kiasi wakati wa ukoloni licha ya kuhujumiwa katika elimu na viongozi waliokuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Uislamu unakua walipambana na nguvu ya Dola ya wakoloni.Wakati huu waislamu walianzisha Taasisi mbalimbali za kuwaunganisha na kuupeleka Uislamu mbele.Mfano East African Muslim Welfare Society (EAMWS) na AMNUT.
Katika kipindi hiki Uislamu ulianza kudhoofishwa kitaalamu na waislamu kuanza kuritadishwa.Hali ya waislamu wa sasa ni matokeo ya hujuma za wakoloni wa kikristo dhidi ya Waislamu na Uislamu.
Nguvu ya Uislamu baada ya ukoloni ilizidi kuwa duni kwani hujuma za wakoloni dhidi ya Uislamu zilirithiwa na watala wengine waliofuata.Uislamu haukupewa nafasi ya Kujiimarisha na waislamu waliundiwa vyombo vya kuwadhibiti, rejea ukurasa 427-432 kitabu cha EDK kidato cha nne.Viongozi wa Kiislamu walikamatwa na kuwekwa vizuizini na pia mipango yao ya elimu ilihujumiwa kwa makusudi.Rejea hujuma dhidi ya EAMWS na mkakati wake wa kuanzisha chuo kikuu cha Kiislamu mwaka 1964.(Ukurasa wa 417-424 Edk kidato cha nne).
Hata hivyo waislamu waliendelea na jitihada za makusudi kukabiliana na changamoto zinazowakabili kwa kuanza kuweka mikakati ya kuwanyanyua na kuirudisha nguvu ya waislamu.
Nguvu ya upinzani dhidi ya Uislamu Tanzania na Afrika Mashariki
Upinzani dhidi ya Uislamu Afrika ya Mashariki
Pamoja na udhaifu wa waislamu kiutekelezaji kutokana na mafunzo na mbinu duni za kufundishia Uislamu, bado wamishionari (wa kikiristo) na wakoloni mapema waliona Uislamu utakuwa kikwazo kwao.
Mapema hata kabla ya kuja wakoloni Afrika ya Mashariki mikakati ya kuupiga vita Uislamu na kueneza ukristo iliwekwa.
Katika mkutano wa Berlin wa 1884 wa kugawana Bara la Afrika, ukiristo ulipewa hadhi maalumu. Walikubaliana katika mkutano huo kuwa Dola zote za kikoloni zitoe hifadhi maalumu kwa makanisa.
Chama cha White Fathers kilianzishwa na Kadinal Lavingire kwa lengo maalumu la kuupiga vita Uislamu na kueneza ukristo Afrika ya Mashariki.
Serikali za kikoloni za Mjerumani na Muingereza ziliweka bayana azma ya kuupiga vita Uisalmu. Kamishna Sr. H. Johnston (1899 1901)alimuandikia D.C. wa Busoga Uganda kutokana na malalamiko ya Askofu Tuchor juu ya kuenea Uislamu kuwa:
“Haikuwa kwa maslahi ya Serikali ya Uingereza iwapo Uislamu utapata wafuasi wengi kwani kwa asili yao waislamu ni wagumu kuwatawala na katika nyoyo zao wanapinga utawala wa dola ya kikristo.”
Na akawaonya machifu wafanye kila njia ya kuupiga vita Uislamu.
Huko Uganda katika mikakati yao ya kuudhofisha Uislamu na waislamu walifanya yafuatayo:-
(i) Walizuia Uislamu isienee kusini mwa Sudan ili Uganda isiathiriwe sana na Uislamu,Uislamu ubakie tu kwenye pwani ya Kenya na Tanzania.
(ii) Kuzibana juhudi za kueneza Uislamu.
(iii) Kuwanyima waislamu fursa ya Elimu kwa mfano:(a) 1944 Waislamu wa Uganda walipewa £ 213 tu na serikali kwaajili ya elimu yao ambapo wakiristo walipewa £ 134,000.
(b) Utafiti wa Dr. Malekela wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam wa 1983 ulionesha kuwa kati ya wanafunzi wanaosoma shule za Sekondari za serekali Tanzania 78% ni wakristo na 22% ni waislamu.
Tafsiri ya hatua hizi ni kwamba Uislamu uliokuja Afrika Mashariki miaka 1000 iliyopita ukawa unadumaa na Ukristo uliokuja Afrika Mashariki miaka 100 tu iliyopita ukawa unazidi kustawi na kutawala.
Katika kueneza Ukristo na kuwaritadisha waislamu,wakristo walibuni mbinu zifuatazo:
Walificha uhasama na chuki zao dhidi ya Uislamu
walizokuwanazo mwanzoni na badala yake wakajenga urafiki wa kinafiki na waislamu kwa kuwatembelea,kuwapa zawadi na kuchanganyika nao katika misiba, harusi n.k. Waislamu wengi kwa kutojua dini yao vizuri na lengo walighilibika na kuritadishwa. Rejea D.W.W. Jz.6 uk 350. Mradi maalumu wa kuritadisha Waislamu ulianzishwa (Islam in Afrika Project) na makao yake makuu yalikuwa Nairobi.
Wakristo walijitahidi sana kuingia vijijini na kujenga makanisa, shule na hospitali wakati waisalmu waliishia mijini. Matokeo yake wakristo wametapakaa vijijini Afrika Mashariki nzima, ambapo waislamu wanabakia mijini tu.
Wakristo wana umoja na mipango madhubuti ya muda mfupi na mrefu ya kufikia lengo lao la kutawala jamii kinyume na Waislamu ambao ndio wenye dhima ya kuutawalisha Uislamu katika jamii hawana hata fikra juu ya hilo.
Kupigwa vita Uislamu Tanganyika.
Wafanya biashara wa kiarabu waliokuwa waislamu waliwatangulia watawala wa Kijerumani (wakristo) kwa karne 10.
Wafanya biashara wa kiarabu hawakuwa na lengo la kutawala, bali kila walipoweka makaziyao katika miji ya pwani na bara walijenga msikiti na kuanzisha madrasa (Quranic School).
Kama tulivyoona, utawala wa kikoloni wa Wajerumani uliambatana na ukristo, hivyo pamoja na ukatili waliokuwa wakiwafanyia wanyeji wa Tanganyika kwa ujumla, walizidisha ukatili wao dhidi ya waislamu na kebehi dhidi ya dini yao.
Kwa sababu hii Machifu Waislamu wakawa katika mstari wa mbele kupambana na Wajerumani.
Bushiri wa Pangani alipambana na wajerumani 1888 – 1889 baada ya mbwa wa mzungu kuingia msikitini katika mwezi wa Ramadhani.
Chifu Mkwawa 1894 alianzisha vita vya Jihad dhidi ya watawala wa kijerumani na wamishenari.
1892 Chifu Isike wa Unyanyembe, Tabora aliendesha jihadi dhidi ya watawala wa kijerumani na wamishenari.
Vita vya Maji Maji vilivyoendeshwa na viongozi waislamu akina Ali Songea, Suleiman Mamba n.k. vilikuwa jihad dhidi ya wakoloni wa kijerumani na wamishenari.
Wakoloni wa Kijerumani walipoingia Tanganyika walijiimarisha kwanza kwenye miji ya pwani.
Waliwakuta wenyeji wa pwani wanajua kusoma na kuandika kwa kutumika herufi za kiarabu na wakawatumia katika shughuli za utawala – Maakida na Maliwali wakawa ni waislamu.
Walianzisha shule za kwanza Bagamoyo na Tanga na wanafunzi wa kwanza wa shule hizi wakawa ni waislamu (Rejea uk 108 – A short history of Tanganyika)
Wakristo wa kaja juu kumshutumu Gavana Von Soden kuwa anaendesha sera za kuwapendelea Waislamu.
Kutokea hapo (baada ya shutuma hii) Serikali ya kikoloni ya mjerumani ikaanza kuendesha sera ya kuwabagua waislamu katika elimu na kuwapendelea wakristo huku wote wakilipa kodi sawa kwa serikali. Sera hii iliendelezwa na serikali ya kikoloni ya Waingereza.
Udhalili wa waislamu kielimu Tanganyika unadhihirishwa kwa vielelezo na Sheikh Salim Kianga katika makala yake katika gazeti la Kiongozi la 26/10/1956 uk. 3 Rejea D.W.W. Jz. 6, uk. 352 -353.
Katika miaka ya 1950, sehemu mbalimbali nchini – Waislamu walikuwa wakidai utawala wa kikoloni, uwaruhusu nao waanzisheshule. Kutokana na msimamo wa waislamu ilibidi waruhusiwe kwa masharti mengi na magumu – hii angalau iliwawezesha waislamu kuwa na shue 28 za msingi,1956 kwa nchi nzima – rejea makala ya S.Kiangi.
Katika kuanzisha shule hizi wazee wetu walijitoa muhanga kwa:
Pamoja na hali ngumu ya uchumi wakati ule, walitoa michango ya fedha katika kujenga na kuendesha shule hizi.
Walijitolea nguvu kazi katika kujenga shule hizi
. (iii) Waliwaasa vijana wao kuchukua Ualimu na kurejea kufundisha katika shue ya Muslimu – Rejea Maelezo ya Mwl. Hamis Njaritta.
Novemba, 1958 Waislamu walikutana Dar es salaam katika mkutano waliouita” Africa Muslim Education conference.” Katika mkutano huu Waislamu waliorodhesha malalamiko yao dhidi ya serikali ya kikoloni kuhusiana na ubaguzi wa elimu. Miongoni mwa malalamiko yao ni:
(i) Mara ya waislamu walipoanza kufungua shule serikali ya kikoni iliweka katika Mpango wa Elimu wa Miaka Mitano (F.Y.E.P) kuwa isifunguliwe shule ya msingi tena.
(ii) Pale ambapo waislamu wamefungua shule hulazimishwa wafundishe Qur’an tu, vinginevyo
wanashitakiwa.
(iii)Shule za Muslimu ambazo zimekubaliwa na serikali zinanyimwa misaada (Grant in Aid) wakati waisalmu wanalipa kodi serikalini sawa na Wakristo.
Mchango wa Waislamu katika kuleta uhuru Tanganyika
Wakoloni, kama tulivyoona walilidhoofisha kundi la waislamu kielimu na kulipendelea kundi la wakristo na kuliweka karibu nao ili walitumie katika utawala.
Waislamu walidhihirikiwa na ubaguzi na uonevu huo na ikawa ndio kichocheo cha kujitoa muhanga katika kupigania Uhuru Tanganyika.
Kama tulivyoona, harakati za mwanzo za kupambana na Serikali ya kikoloni zilizoongozwa na Chifu Mkwawa wa Uhehe, Kalenga, Iringa,
Chifu Isike wa Unyanyembe, Tabora, na vita vya Maji Maji vilivuyoongozwa na akina Ali Songea na Suleiman Mamba (Kinjekitile), zilianzia katika maeneo ya Waislamu wakichukulia vita vile ni jihadi dhidi ya maadui wa Uislamu na Waislamu. Wakristo walishirikiana na wakoloni kupambana na Watanganyika wenzao.
Kati ya mika ya 1939 na 1947 yalitokea machafuko na migomo katika sehemu za kazi na hasa katika bandari za Tanga na Dar es salaam kupinga dhuluma za kikoloni. Waliongoza migomo hii walikuwa waislamu mpaka pakapatikana mwanya wakuanzisha vyama vya wafanyakazi vya kijamii.
Katika kutumia mwanya huu Waislamu walianzisha:
- Al-Jamiatul Islamiyya fiy Tanganyika
- Da’awat Al-Islamiyya
Tanganyika African Association (TAA) iliyo asisi TANU, ilianzishwa 1929 na viongozi wake wakawa ni wale wale wa jumuia hizo mbili za Waislamu.
Nyerere alikaribishwa na waislamu na kupewa uongozi katika harakati za kisiasa katika hatua za mwanzo za kuanzishwa kwa TANU 1954.
Kuingia kwa Nyerere na wasomi weninge wa kikristo katika TANU kulibadili sura ya Siasa Tanganyika.
Kwa vile wakristo ndio wengi waliokuwa wasomi, walishika nafasi nyeti katika uongozi wa chama k.m. mwenyekiti alikuwa Nyerere,Makamu wake akawa John Rupia, wote wakatoliki.
Muelekeo huu uliwatisha baadhi ya Waislamu kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa wakristo hao kutotenda haki kinyume chake wakatumia nafasi zao kuendeleza dhuluma ile ile ya wakoloni dhidi ya Waislamu na Uislamu.
Sheikh Suleiman Takadiri aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la TANU alikuwa wa mwanzo kuonesha wasiwasi wake. Nyerere aliongoza vita dhidi yake na akaongoza kutengwa kwake na hata waislamu wenzake. Nyerere akamwita “Suleiman Mtaka Dini,” anayechanganya dini na siasa. Sheikh Takadiri alibakia na msimamo wake mpaka kufa kwake na aliwaambia waislamu watayakumbuka maneno yake katika siku za usoni.
Baadhi ya waislamu walipoteza Imani na TANU na kuanzisha chama cha siasa cha kiislamu kilichoitwa “All-Muslim National Union of Tanganyika” (AMNUT) mnamo 1957 – lengo la AMNUT lilikuwa kupigania haki kwa wote. Kilipigwa vita na Nyerere na kutoweka.
Wakati waislamu wanaacha agenda yao ya kusimamisha Ukhalifa katika jamii na kufuata sera ya “kutochanganya dini na siasa” Mwl. Nyerere alikuwa akiandaliwa kisirisiri na masharika ya kikristo ili aje kusimika utawala wa kikatoliki Tanganyika.
Kufuatia safari ya Mwl. Nyerere ya Umoja wa Mataifa mwaka 1956 ambayo kwa kiwango kikubwa alisaidiwa na shirika la kikatoliki la Maryknoll Fathers, Serikali ya kikoloni ililalamikia Vatican. Padre William Collins aliyekuwa katibu Mkuu wa shirika hilo la Maryknoll, 1957 aliiandikia Vatican ripoti maalum. – Rejea sehemu ya ripoti hii D.W.W Jz. 6 uk 356 – 357.
Pamoja na kumuandaa Nyerere, Maryknoll Fathers na White Fathers walikuwa wakiandaa watu wengine ili wajeshika nafasi muhimu
serikalini baada ya Uhuru. Rejea kauli ya padri Paul Crane aliyeitembelea Tanganyika, 1959:-
“Lazima tujitahidi kadiri ya uwezo wetu kupata wasomi wakatoliki ambao watashika nafasi muhimu kwenye ngazi zote za kijamii. Wakatoliki wajitahidi kushika nafasi hizi. Tutawezakuwaingiza kwenye nafasi za uongozi kwa njia ya kujenga vikundi vidogo vidogo vya wasomi wakatoliki” (Paul Crane,
Rome:CIPA, 1960).
Kutokana na maandalizi hayo, wakristo walihodhi nafasi zote nyeti za uongozi katika serikali baada ya uhuru, serikali ikawa inaendeshwa kwa matakwa na matashi ya Kanisa Katoliki.
Nyerere kwa maandalizi aliyoyapata akishirikiana na watawala wenzake wakristo alikuja kuwa kiungo muhimu kati ya kanisa na serikali na kulipa kanisa nafasi nzuri ya kuwadhulumu na kuwapiga vita Waislamu na Uislamu: Rejea ahadi ya Nyerere kwa katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Father Robert Rweyemamu, kuwa:
“………..I want to give the Church a better chance here so that she will not be blamed as in the Catholic countries” (Jan P. Van Bergen,pg. 335, 1981).
Tafsiri
“ ………. Nataka kulipa Kanisa (Katoliki) nafasi nzuri hapa (nchini) ili lisilaumiwe kama linavyolaumiwa hatika nchi za kikatoliki” (Jan P. Van Bergen,pg. 335, 1981).
Hivyo, wakati Waislamu walipigania uhuru huku wameghilibika na kuitupa agenda yao ya Uislamu, Wakristo walikuwa wakijiandaa kuja kushika serikali katika mazingira ambayo yatawewezesha kupambana na Uislamu, na kweli walifanya hivyo mara tu baada ya Uhuru.
Mkutano wa kwanza wa Waislamu baada ya Uhuru, 1962
Uhuru wa Tanganyika ulipatikana 9 Dec.1961. Mwaka uliofuatia, 1962, Waislamu walikutana nchi nzima kujadili nafasi ya Uislamu katika Tanganyika huru. Taasisi zilizohudhuria mkutano huo zilikuwa:
(i)East African Muslim welfare Society (EAMWS)
(ii) Da’awat Islamiyya
(iii) Al-Jamiatul Islamiyya fiy Tanganyika
(iv) Muslim Education Union
Pamoja na mambo mengine, mkutano uliazimia kuanzishwa Idara ya Elimu chini ya EAMWS.Waislamu waliamua warekebishe wenyewe upogo uliokuwepo wa elimu kati ya waislamu na wakristo.
Harakati za kujenga shule Tanganyika nzima zilianza na mikakati ilikuwa inafanyika ya kujenga Chuo Kikuu cha kwanza kwa waislamu katika Afrika Mashariki.
Nyerere Mkatoliki aliyeahidi kuwa atalipa kanisa lake nafasi ya (upendeleo wa) pekee, hakufurahishwa na umoja na maendeleo ya waislamu hasa katika sekta ya elimu.
Mwaka 1963, Nyerere alitangaza kutaifishwa mashule yote ya msingi na sekondari ya misheni na Muslim kwa kisingizio kuwa ni katika kuwasaidia waislamu ambao walikuwa na shule chache sana za sekondari nyingi zikiwa za Aga Khan.
Shule za Seminari za Msingi na Sekondari za Wakristo zilibakia kuendeshwa na makanisa husika. Pia shule za Serikali zilitaifishwa kwa kuendeshwa na serikali kifedha lakini uongozi wa shule hizo ulibakia chini ya uongozi wa wakristo ambao walihakikisha kuwa waislamu hawapati nafasi katika shule hizo ila kwa asilimia chache tu (10 - 20%).
Harakati za Waislamu za kujenga mashule na kuendeshazilizoshamiri katika miaka ya 1950 mpaka kupata Uhuru, zikaishia pale wakitarajia kufaidi matunda ya uhuru, hasa wakizingatia hutuba ya Nyerere aliyoitoa bungeni tarehe 10 Dec.1962, wakati Tanganyika inakuwa Jamuhuri - Rejea D.w.w. Jz. 6, uk. 359.
Kwa hutuba ile, Waislamu waliamini kuwa serikali yao iko katika mchakato wa kubadilisha hali.
Nyerere pamoja na kutaifisha shule, hakuwa ameridhika na mshikamano wa waislamu chini ya EAMWS.
Katika mkutano wa EAMWS wa 1963, Nyerere kwa kuwatumia wajumbe wanafiki aliandaa mazingira ya kusambaratisha umoja huu ili aunde chombo cha Waislamu atakachoweza kukidhibiti.
Viongozi wa EAMWS, kwa uwezo wa Allah (s.a) waling’amua njama za Nyerere na wakadhibiti mkutano ule na wajumbe wote, ukiacha wale wanafiki, wakakataa kata kata kuvunja umoja wa Waislamu.
Nyerere alialikwa kufunga mkutano ule na waislamu wakapata fursa ya kumueleza kuwa waislamu hawakotayari kuvunja umoja wao ambao ni faradhi kwao na pia walimuonesha uadui unaofanywa na serikali yake dhidi ya Uislamu.
Nyerere baada ya kuona ameumbuka aliamua kudhihirisha uadui wake dhidi ya Uislamu kwa kufanya yafuatayo:
(i) Aliwaandama viongozi wa E.A.M.W.S waliokuwa rafiki zake wa kisiasa wakati wa kupigania uhuru nao ni Tewa Said Tewa – Rais wa E.A.M.W.S, Bibi Titi Mohamed – makamu wa Rais wa E.A.M.W.S na Chifu Abdallah Said Fundikira aliyekuwa Rais wa E.A.M.W.S. kwa upande wa Tanganyika. Aliwaondoa katika uongozi wa serkali na siasa na kuwazulia kashfa mbalimbali.
(ii) Palipotokea kuasi kwa jeshi la “Tanganyika Rifles”, 1964, Nyerere alitumia fursa ile na kuwatia kizuizini viongozi wengi wa kiislamu ambao katika kesi ya uhaini hawakuonekana kuhusika kabisa.
(iii) Aliwafukuza nchini masheikh wengi waliokuwa mstari wa mbele katika harakati za kuendeleza Uislamu wakiwemo.
Sheikh Hassan bin Amir
Sheriff Hussein na mdogo wake Sheikh Mwinyibaba
(iv) Mwaka 1964, vile vile alivunja Baraza la Wazee la TANU ambalo lilikuwa na wajumbe waislamu watupu na ambalo lilikuwa linashikiza chama na serikali yake itekeleze ahadi ya kurekebisha hali ya Waislamu na kuonesha uadui onaofanywa na serilai dhidi ya Uislamu.
(v) Nyerere alizima juhudi za kuanzishwa Chuo Kikuu cha Waislamu wa Afrika ya mashariki kilichoahidiwa kujengwa na serikali ya Misri. Nyerere alimshawishi Gamal Abdul Nasser, ajenge madrasa badala ya Chuo Kikuu, pale Changombe ambayo mpaka sasa ipo na inaendeshwa na serikali ya Misr.
(vi) Nyerere kwa kutumia Waislamu vibaraka (kama akina Adamu Nasibu na wenzake) na vyombo vya dola, alivunja umoja wa waislamu na kuanzisha BAKWATA – Tanzania Muslim Suppreme Council 1968.
Lengo la BAKWATA ni kuwadhibiti waislamu wa Tanganyika wasifanye maendeleo yatakayopelekea uislamu kusimama katika jamii. Lengo hili walilithibitisha viongozi wake:
(i) Sheikh Hemed bin Juma Hemed aliyekuwa Muft wa kwanza wa BAKWATA alitamka wazi kule Shinyanga, 1992, wakati wa vugu vugu la kuanzishwa Baraza kuu la Jumuia na Taasisi za Kiislamu, kuwa BAKWATA iliundwa ili kudhibiti harakati za kiislamu.
(ii) Sheikh Mohamed Ali, aliyekuwa katibau Mkuu wa kwanza wa BAKWATA aliwaeleza vijana wa Warsha ya waandishi wa Kiislamu” baada ya mapinduzi ya uongozi wa BAKWATA ya 1979/82, kuwa BAKWATA ilikuwa haiwezi kufanya jambo lolote la maendeleo mpaka Nyerere alipe kibali kabla Halimashauri kuu ya BAKWATA haijafikishiwa jambo hilo. Na hapakuwa na jambo lolote la kuendeleza Uislamu lililokuwa linaruhusiwa kufanywa na yeyote bila ya kibali cha BAKWATA ambayo haiwezi kutoa kibali hicho mpka Nyerere atoe kibali hicho au akatae. Nyerere naye alikuwa hatoi kibali hicho mpaka apate ushauri wa kanisa lake.
Kwa mlolongo huu BAKWATA ni chombo cha kanisa katoliki cha kudhibiti maendeleo ya Uislamu. Hili lilidhihirika kwa uwazi mwaka 1981, Sheikh Ahmad Deedat alipoitembelea Tanzania. Sheikh Ahmad ambaye alikuwa marufu kwa mihadhara ya Bibilia, alitoa muhadhara juu ya “Muhammad in the Bible” katika ukumbi wa Lumumba, Dar es Salaam. Kabla hajatoa muhadhara mwingine ambao ulikuwa ufanyikie katika ukumbi wa Diamond, iliandikwa barua na Baraza la Maaskofu (TEC) wakishirikiana na Baraza la Kikristo Tanzania (CCT)kwa katibu Mkuu wa BAKWATA, kuwa asitishe Muhadhara ule
kwa sababu utavuruga imani za waumini wao. Vijana wa MSAUD, waliokuwa wenyeji wa Sheikh Ahmad Deedat, walimkatalia, katibu wa BAKWATA, Al-Maruhum Sheikh Mohamed Ali, ombi lile. Kwa kukatailiwa ombi lile, Sheikh alionesha kuwa na khofu na kuwaambia vijana:-
“Nyinyi ni vijana wadogo, hamfahamu nguvu na vitimbi vya viongozi wa Kanisa katika nchi hii. Nakuhakikishieni kuwa hili linashughulikiwa na serikali. Tunaweza kupata malipo yake. Hili sio ombi bali ni amri”.
Jitihada za kuhuisha Uislamu Tanzania na Afrika Mashariki hivi leo
(i)Kuanzishwa kwa seminari ya Masjid Qubah 1983.
(ii)Kuibuka kwa seminari nyingi za Kiislamu.
1989 Ununio Boys High School na Kunduchi Girls High School.
1992 Ubungo Islamic High School.
Mudio Islamic Secondary School.
Kirinjiko Islamic Secondary School.
(iii)Kuanzishwa kwa vyuo vya ualimu na chuo kikuu.
Al-Haramain Teachers’ Colledge 1987.
Ubungo Islamic Teachers’ Colledge 1998.
Kirinjiko Islamic Teachers’ Colledge 2004.
Ununio Islamic Teachers’ Colledge 2010.
Muslim Univesity of Morogoro (MUM) 2005.
(IV)Kuanzishwa Baraza Kuu 1992
(v)Kamati za Kuendeleza Uislamu, 2003
Mwaka 2003, waislamu wanaharakati kutoka kote nchini walikutana Kirinjiko, Same na kuasisi kundi la Harakati kwa jina la “Kamati ya Kuendeleza Uislamu Tanzania”, kwa ufupi KKUT itakayokuwa na uongozi kuanzia ngazi ya mtaa hadi Taifa. KKUT katika kila ngazi inawajumuisha waislamu wote wanaofanya jitihada za makusudi za kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii. Kamati za kuendeleza Uislamu hazina ubaguzi wa kitaasisi au wa aina yoyote. Muislamu yeyote aliyetayari kushiriki kwa mali yake na nafsi yake katika harakati za kuuendeleza Uislamu kwa lengo la kuudhihirisha na kuutawalisha katika jamii anakuwa ni mwanakamati. Ili kupata wanakamati wenye sifa stahiki zinafanyika semina za uamsho kuanzia ngazi ya Taifa hadi Mtaa na kumewekwa mikakati ya kuwa na darasa duara kila mtaa. Kazi kubwa ya kuanza na ya msingi ya kamati za kuendeleza Uislamu ni kutoa elimu sahihi ya Uislamu na kusimamia utekelezaji wake katika kuyaendea maisha ya kila siku ya kibinafsi na kijamii. Ili hili lifanikiwe kamati za kuendeleza Uislamu katika kila ngazi zimeazimia kufanya yafuatayo:
(i) Kuanzisha na kuendesha vituo vya elimu kuanzia shule za awali hadi vyuo vya ualimu.
(ii) Kuanzisha na kuendesha Chuo Kikuu cha Kiislamu kitakachotoa elimu ya fani zote za elimu ya mazingira na mwongozo.
(iii)Kusimamia ufundishaji wa Elimu ya Dini ya Kiislamu katika shule zote za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu kote nchini.
(iv)Kuwahamasisha na kuwaandaa walimu wote waislamu kufundisha somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu katika shule zao za msingi,sekondari na vyuo vya ualimu.
(v) Kufanya jitihada za makusudi za kuandaa nguvu kazi ya kuendesha harakakati za kiislamu kutokana na wanafunzi wa sekondari, vyuo vya ualimu na vyuo vikuu nchini na nje ya nchi.
(vi)Kujiimarisha kiuchumi kwa kuanzisha na kuendesha mifuko na miradi ya kiuchumi.
(vii)Kuweka mipango ya muda mfupi na mrefu katika kutekeleza majukuu sita yaliyoainishwa hapo juu na kufanya tathmini kitaifa kila baada ya miezi sita.
Katika kufanya juhudi za kuhuisha harakati za kiislamu kuna mambo muhimu yakuzingatia:
(i) Wanaharakati hawana budi kutambua kuwa kikwazo kikuu cha maendeleo ya Uislamu na mshikamano na umoja, si BAKWATA au wingi wa Taasisi, au ….. bali ni serikali ya mfumo katoliki.
(ii) Nyenzo kuu itakayopelekea kusimamisha Uislamu katika jamii ni Elimu ya Mazingira na muongozo.
Kwa mazingatio haya, harakati za kuhuisha Uislamu katika jamii tutazipima kwa kuangalia ni jinsi gani tunasimamia elimu ya mazingira na mwongozo na jinsi gani tunachukua tahadhari na serikali ya mfumo Katoliki ili isitukwamishe tena.
“Mola wetu,Tunaomba hifadhi ya Nuru ya uso wako,nuru iangazayo mbinguni na kuondosha aina zote za giza na nuru iongozayo na kudhibiti mambo yote ya hapa duniani na akhera.Tupe uongofu utokao kwako na tutengenezee uongofu katika jambo letu”.”Amin”.
Wabillah Tawfiiq